TEHRAN (IQNA)- Katika safari yake ya kwanza nchini Morocco tangu nchi hiyo ya Kiafrika ianzishe uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala huo ghasibu amefungua rasmi ofisi za ubalozi wa utawala huo mjini Rabat.
Habari ID: 3474185 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/13
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amelaani vikali safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel nchini Morocco na kubainisha kuwa, ziara hiyo haikubaliki.
Habari ID: 3474182 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/12
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali kikao cha wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Harakati ya Ukombozi ya Palestina (PLO), mawaziri na maafisa wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na viongozi wa utawala haramu wa Israel chenye lengo la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3474168 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/07
TEHRAN (IQNA) - Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na walowezi wa Kizayuni walikiuka haki za Wa palestina katika zaidi ya mara 3,800 mwezi Julai katika katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na mjini al-Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3474162 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/05
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameitaka Saudi Arabia iwaachilie huru mahabusu wote Wa palestina inaowashikilia na kufunga faili lao.
Habari ID: 3474161 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/05
TEHRAN (IQNA)- Nchi 14 za Afrika zimetangaza msimamo imara wa kupinga utawala wa haramu wa Israel kuwa mwanachama mtazamaji katika Umoja wa Afrika
Habari ID: 3474149 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/01
TEHRAN (IQNA)- Nchi kadhaa za Afrika zinaendelea kupinga hatua ya utawala haramu wa Israel kuidhinishwa kuwa ‘mwanachama mwangalizi’ wa Umoja wa Afrika.
Habari ID: 3474140 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/30
TEHRAN (IQNA)- Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema mashambulio yaliyofanywa na jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika vita vya siku 11 dhidi ya Ukanda wa Ghaza yalifikia kiwango cha jinai za kivita.
Habari ID: 3474134 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/28
TEHRAN (IQNA)- Walowezi wa Kizayuni waliokuwa wakilindwa na kusindikizwa na askari wa utawala haramu wa Israel leo wameuvamia tena msikiti wa Al Aqsa katika mji mtukufu wa Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3474132 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/27
TEHRAN (IQNA) - Mwanamichezo wa mchezo wa Judo kutoka Sudan Mohamed Abdalrasool amekuwa mwamichezo wa pili kukataa kucheza na Muisraeli Tohar Butbul katika michezo ya Olimpiki 2020 ya Tokyo.
Habari ID: 3474130 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/26
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali uamuzi wa Umoja wa Afrika kuupa utawala haramu wa Israel hadi ya ‘mwangalizi’ katika taasisi hiyo ya nchi za Afrika.’
Habari ID: 3474122 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/24
TEHRAN (IQNA)- Mwanamichezo wa mchezo wa Judo wa Algeria ameamua kujitoa kwenye michezo ya Olimpiki ya 2020 Tokyo inayofunguliwa rasmi leo katika mji mkuu huo wa Japan, ikiwa ni harakati ya kutangaza mshikamano na Palestina na kupinga kuanzishwa uhusiano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3474120 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/23
TEHRAN (IQNA) - Shirikisho la Soka la Palestina limekaribisha hatua ya FC Barcelona ya Uhispania kukataa kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Beitar ya utawala haramu wa Israeli katika mji wa Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3474112 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/18
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imetoa wito kwa umma wa Palestina kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya Itikafu ndani ya Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) kwa lengo la kulinda eneo hilo takatifu ambalo linakabiliwa na hujuma ya walowezi wa Kizayuni wanaopata himya ya utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3474110 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/18
TEHRAN (IQNA)- Wafungwa watano Waplaestina wameanza mgomo wa kususia chakula katika magereza ya kuogofya ya utawala wa Kizayuni wa Israel kama kwa lengo la kulalamikia kushikiliwa gerezani bila ya kubainika makosa yao.
Habari ID: 3474105 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/16
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) Ismail Haniya na Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina Ziad al Nakhala wamempongeza rais mteule wa Iran Sayyid Ebrahim Raeisi kwa ushindi wake katika uchaguzi wa rais.
Habari ID: 3474098 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/14
TEHRAN (IQNA)-Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imewataka wakazi wa Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan kudumisha mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuhakikisha kwamba ardhi ya Palestina inakuwa kaa la moto kwa maghasibu hao.
Habari ID: 3474092 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/11
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amesisitiza kuwa nchi yake itaendelea kuunga mkono haki za kisheria za Palestina na katu haitafanya mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3474087 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/10
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma salamu za rambirambi kwa taifa la Palestina kutokana na kufariki dunia Katibu Mkuu wa Kamandi Kuu ya Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina (PFLP—GC), Ahmad Jibril.
Habari ID: 3474083 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/09
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za rambirambi kufuatia kuaga dunia mwanamapmbano maarufu wa Palestina, Ahmed Jibril.
Habari ID: 3474082 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/08