iqna

IQNA

Misikiti katika eneo la Ukanda wa Ghaza katika ardhi za Palestina imesafishwa kwa dawa za kuua virusi kabla ya kufunguliwa baada ya kufungwa kwa miezi miwili ili kuzuia kuenea kirusi cha corona.
Habari ID: 3473283    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/22

Mkuu wa ICRO
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Uhusiano wa Kiislamu Iran (ICRO) amesema, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) inapaswa kutekeleza majukumu yake kuhusiana na Fatuwa ambayo imetolewa na wanazuoni wa Kiislamu ya kuharamisha kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473281    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/21

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Ukuras wa Twitter wa Kiongozi Maudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu umezungumzia hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473280    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/21

TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Palestina amelaani kitendo cha kuruhusiwa ujumbe wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuingia ndani ya Msikiti wa al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) huku Wa palestina wakizuiwa kuswali katika msikiti huo.
Habari ID: 3473279    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/20

TEHRAN (IQNA)- Wananchi wenye hasira nchini Bahrain wameandamana kupinga safari ya ujumbe wa Marekani-Kizayuni katika nchi yao kwa lengo la kutangaza rasmi mapatano ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida kati ya Bahrain na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473276    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/19

TEHRAN (IQNA) - Asilimia 95 ya wananchi wa Bahrain wanapinga hatua ya utawala wa kifalme nchini humo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473272    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/18

TEHRAN (IQNA)- Sayyid Ammar Hakim, Kiongozi wa Mrengo wa Kitaifa wa al-Hikma wa Iraq amelaani vikali siasa za baadhi ya mataifa ya Kiarabu katika eneo la Asia Magharibi za kufanya mapatano na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kwamba, nchi yake katu haitafanya mapatano na utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3473271    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/18

TEHRAN (IQNA) – Makumi ya walowezi wa Kizayuni siku ya Alhamisi waliuhujumu uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) wakiwa wanalindwa na askari wa utawala haramu wa Israel ambapo wametekeleza ibada za Kiyahudi katika eneo hilo takatifu la Waislamu.
Habari ID: 3473265    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/16

TEHRAN (IQNA) – Utawala wa Kizayuni wa Israel umeidhinisha ujenzi wa nyumba mpya 2,166 za walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3473263    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/15

TEHRAN (IQNA) – Mtaalamu maarufu wa kisiasa Kuwaita amelaani hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia na Israel na kutaja hatua hiyo kuwa sawa na ukoloni mamboleo.
Habari ID: 3473257    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/13

TEHRAN (IQNA)- Hali ngumu na isiyo ya kibinadamu ya magereza ya utawala wa Israel imepelekea mateka au wafungwa kadhaa kususia chakula kama njia ya kubainisha malalamiko yao.
Habari ID: 3473252    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/12

TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) na Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) imemkosoa vikali balozi wa zamani wa Saudi Arabia nchini Marekani kutokana na matamshi yake dhidi ya wapigania ukombozi wa Palestina.
Habari ID: 3473247    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/10

TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Sudan amekosoa hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema, hatua hiyo ni usaliti kwa kadhia ya Palestina.
Habari ID: 3473243    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/09

TEHRAN (IQNA) – Wasomi wa Kiislamu na wanaharakati katika mirengo kadhaa ya Palestina wamelaani vikali mapatano ya kuanzishwa uhusiano baina ya Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu.
Habari ID: 3473238    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/07

TEHRAN (IQNA) – Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammad bin Salman, ameutembelea utawala wa Kizayuni wa Israel mara kadhaa kwa siri, amefichua afisa wa zamani wa usalama katika utawala huo.
Habari ID: 3473237    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/07

TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kizayuni umeamua kujenga maelfu ya nyumba za walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wa palestina unazoendelea kupora huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3473235    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/06

TEHRAN (IQNA) – Wananchi wa Bahrain wameandamana tena Ijumaa katika mji mkuu Manama na miji mingine kupunga hatua ya utawala wa kifalme nchini humo kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473228    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/03

TEHRAN (IQNA) – Wanaharakati wa kisiasa nchini Tunisia wametaka Oktoba Mosi itambuliwe nchini humo kama ‘Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Uzayuni.’
Habari ID: 3473224    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/02

TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imepinga madai ya afisa mwandamizi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuwa eti utawala bandia wa Israel umesitisha upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni baada ya utawala huo kuanzisha uhusiano na nchi mbili za Kiarabu za UAE na Bahrain.
Habari ID: 3473222    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/02

TEHRAN (IQNA) - Jumuiya Kuu ya Fiqhi ya Kiislamu ya Sudan imetoa fatwa ya kuharamishwa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473220    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/01