TEHRAN (IQNA) – Wa palestina katika Ukanda wa Ghaza wamemuenzi Shahidi Luteni Jeneali Qassem Soleimani mwaka mmoja baada ya kuuawa kwake katika hujuma ya jeshi la kigaidi la Marekani katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Habari ID: 3473505 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/29
Jumuiya ya Maulama wa Kiislamu Duniani
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu (IAMS) amesema kuwa, viongozi wanaotaka mapatano wameanzisha uhusiano wa kawaida na Israel kwa sababu ya woga, tamaa na kwa ajili ya kulinda maslahi yao pamoja na tawala zao, hatua ambayo ni haramu na batili.
Habari ID: 3473502 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/28
Harakati ya Kiislamu ya Amal ya Jordan
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Kiislamu ya Amal ya Jordan imetoa taarifa na kusema hatua ya Morocco kuafiki kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kashfa kubwa na pia ni uhaini wa kihistoria.
Habari ID: 3473491 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/25
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kitendo cha baadhi ya nchi za Kiarabu cha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuwasaliti wananchi wa Palestina na umma wa Kiislamu kwa ujumla.
Habari ID: 3473488 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/24
TEHRAN (IQNA) – Indoneisa imekanusha ripoti kuwa iko tayari kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala bandia wa Israel.
Habari ID: 3473487 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/24
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Tunisia imeashiria juhudi za baadhi ya mataifa ya kieneo za kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kwamba, serikali ya Tunis haina mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3473484 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/23
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Wananchi wa Yemen ameashiria kuendelea kuchimbwa mashimo na njia za chini kwa chini kuelekea katika msikiti mtakatifu wa al-Aqswa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu na kueleza kwamba, Waislamu wanapaswa kutumia nyenzo na suhula zote kukabiliana na njama hizo.
Habari ID: 3473483 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/23
TEHRAN (IQNA) -Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, sera za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) za kuunga utawala wa Kizayuni wa Israel ni kwa madhara ya haki za Wa palestina .
Habari ID: 3473477 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/21
TEHRAN (IQNA) Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan amekanusha kuwepo mashinikizo ya aina yoyote ya kuitaka nchi hiyo ijiunge na safu ya nchi zinazofanya mapatano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473474 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/20
TEHRAN (IQNA) – Maelfu ya Wa palestina leo wamshiriki katika Swala ya Ijumaa katika kibla cha kwanza cha Waislamu, yaani Msikiti wa Al Aqsa ulioko mjini Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3473467 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/18
TEHRAN (IQNA) – Mufti wa Quds (Jerusalem) amelaani vikali hatua ya Walowezi wa Kizayuni kuuhujumu Msikiti wa Al Aqsa mjini humo na kuweka nembo ya Kiyahudi ya Menorah katika msikiti huo.
Habari ID: 3473464 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/17
Kufuatia kuongezeka maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 au corona katika Mji wa Ghaza, wakuu wa eneo hilo la Palestina wanatekeleza hatua kali za kudhibiti maambukizi.
Habari ID: 3473460 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/15
Tunisia imesema haina mpango wowote wa kuchukua uamuzi sawa na wa Morocco wa kuanzisha uhusiano na utawala bandia wa Israel.
Habari ID: 3473457 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/15
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Algeria amekosoa hatua ya Morocco kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473450 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/12
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imelaani vikali 'mapatano' ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Morocco na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473448 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/12
TEHRAN (IQNA) - Harakati za kupigania ukombozi wa Palestina zimelaani vikali hatua ya Morocco kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473444 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/11
Mwanazuoni wa Lebanon
TEHRAN (IQNA) – Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu wa Madhehebu ya Shia Lebanon Ayatullah Abdul-Amir Qabalan amelaani vikali jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wa palestina Waislamu na Wakristo na kuongeza kuwa, kuanzisha uhusiano na Israel ni haramu.
Habari ID: 3473429 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/06
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), imelaani vikali kitendo cha utawala haramu wa Israel kumuua shahidi kijana M palestina aliyekuwa na umri wa miaka 14.
Habari ID: 3473427 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/06
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia ameeleza bayana kuwa kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ni sehemu ya ndoto ya muda mrefu ya kisiasa ambayo wamekuwa nayo viongozi wa utawala wa Aal Saud.
Habari ID: 3473426 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/05
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani kauli aliyotoa waziri wa biashara, viwanda na utalii wa Bahrain kuhusu azma ya nchi yake ya kununua bidhaa zinazozalishwa katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwenye Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3473421 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/04