iqna

IQNA

Wanamaji wa jeshi la utawala haramu wa Israel wameiteka nyara meli ya misaada ya Sweden iliyokuwa imebeba misaada ya Wa palestina walio katika eneo linalozingirwa la Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3321135    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/29

Mkuu wa Kamati Kuu ya Kiislamu ya Palestina amewataka Waislamu wahudhurie kwa wingi katika msikiti mtukufu wa al Aqsa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3314849    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/16

Katika hatua ya kushangaza, Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekataa kuuoredhesha utawala haramu wa Israel na ambao unaendelea kuua watoto wa Ukanda wa Gaza, katika orodha ya tawala zinazovunja haki za watoto duniani.
Habari ID: 3312923    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/10

Jeshi la Utawala haramu wa Israel limewaua watoto wapatao 980 katika hujuma zake za hivi karibuni katika Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3311464    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/06/07

Wa palestina katika Ukanda wa Ghaza wameandaa hafla kadhaa kwa mnasaba wa wiki ya kupinga ubaguzi unaotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 2921399    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/03/03

Walowezi wa Kizayuni wameuvamia tena Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Baitul Maqdis.
Habari ID: 2891642    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/24

Chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini kimetangaza kuendeleza sera ya kuunga mkono mapambano ya Wa palestina ambao wanapigania kuikomboa ardhi yao inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 2822420    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/08

Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ameagiza kubomolewa nyumba mpya 400 za raia wa Palestina wa eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Habari ID: 2822419    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/02/08

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kadhia ya Palestina ndiyo yenye umuhimu mkubwa zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kusimama kidete hadi pale malengo ya Palestina yatakapotimia na hapana shaka kuwa vijana watashuhudia siku hiyo.
Habari ID: 2770295    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/27

Waislamu na hata wasiokuwa Waislamu duniani wanaendelea kulaani kitendo cha hivi karibuni cha jarida moja la Ufaransa la Charlie Hebdo kuchora vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtumu Mtukufu wa Uislamu, Mohammad SAW.
Habari ID: 2766561    Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/26

Umoja wa Mataifa umeulaumu vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuendelea kubomoa nyumba za Wa palestina katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi na kusema kuwa, kitendo hicho ni ukiukaji wa haki za kimsingi kabisa za binadamu.
Habari ID: 2615266    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/05

Bunge la Uhispania na Rais wa Slevonia wameunga mkono suala la kutambuliwa rasmi dola la Palestina. Hatua hii inakuja katika wimbi la uungaji mkono wa dola la Palestina.
Habari ID: 1475315    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/19

Kamati ya Sera za Kigeni katika Umoja wa Ulaya imetangaza vikwazo vipya dhidi ya utawala wa Israel kutokana na hatua za utawala huo za kuvuruga usalama wa Baitul Maqdis na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 1475311    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/19

Mabunge ya Uhispania na Ufaransa yamepanga kupigia kura azimio la kulitambua taifa la Palestina, hatua ambayo imekuwa ikichukuliwa ma nchi kadhaa za Ulaya.
Habari ID: 1473023    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/14

Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa, kumeundwa kamati ya uchunguzi kuhusiana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika ukanda wa Gaza.
Habari ID: 1472788    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/13

Kufuatia kuongezeka na kuenea malalamiko ya Wa palestina katika mji wa Quds (Baitul Maqdis) unaokaliwa kwa mabavu, Ghaza na Ukingo wa Magharibi hivi sasa Wa palestina wanaoishi katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu, yaani Israel, nao pia wameandamana.
Habari ID: 1471813    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/10

Ghasia na machafuko mapya yamezuka kati ya askari wa utawala wa kizayuni wa Israel na waandamanaji wa Palestina katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel baada ya utawala huo kufunga Msikiti mtukufu wa al Aqsa.
Habari ID: 1470536    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/06

Sheikh Bilal Shaaban Katibu Mkuu wa chama cha Hizb Tauhid Islami nchini Lebanon amejiunga na wapenda uhuru na haki duniani katika kulaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel kufunga milango ya Msikiti wa Al Aqsa na kuwazuia Waislamu kuswali ndani ya msikiti huo.
Habari ID: 1466340    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/01

Utawala haramu wa Kizayuni, kwa mara ya kwanza leo Ijumaa alfajiri umefungua milango ya Msikiti wa al-Aqsa baada ya kuifunga mwaka 1967. Utawala huo pia umeshadidisha ulinzi katika maeneo ya jirani na msikiti huo, kutokana na hofu ya kuzuka mapambano makali kutoka kwa Wa palestina .
Habari ID: 1465817    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/10/31

Imam Khamenei
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa ushindi wa Ghaza wa mapambano katika vita vya siku 50 na matamshi ya kushindwa utawala wa Kizayuni mbele ya raia waliozingirwa ni ushindi mkubwa na dhihirisho la ahadi na msaada wa Mwenyezi Mungu na ni bishara ya kufikia ushindi mkubwa zaidi.
Habari ID: 1460936    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/10/17