Duru za habari katika Ukanda wa Ghaza zinaarifu kuwa, karibu Wa palestina 1,700 wameshauawa shahidi katika jinai za siku 27 mtawalia za utawala huo katili wa Kizayuni kwenye ukanda huo.
Habari ID: 1435159 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/08/02
Imam Khamenei
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, 'ulimwengu wa Kiislamu kwa kuweka kando hilitalfu zilizopo, utumie uwezo wake wote kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya Wa palestina katika Ukanda wa Ghaza.'
Habari ID: 1434650 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/29
Imam Khamenei
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwamba, ulimwengu wa Kiislamu unapasa kuipatia kipaumbele kikubwa kadhia ya Ghaza.
Habari ID: 1434649 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/29
Baada ya kumalizika muhula wa usitishwaji vita wa muda katika Ukanda wa Ghaza, utawala wa Kizayuni wa Israel umeanzisha tena hujuma zake za kinyama dhidi ya eneo hilo la Wa palestina .
Habari ID: 1433806 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/27
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, harakati hiyo itaendelea kuwaunga mkono wananchi madhlum wa Palestina na muqawama wao na kwamba harakati hiyo haitasita hata kidogo kutoa msaada wowote unaohitajika katika kupambana na adui Wazayuni.
Habari ID: 1433637 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/26
Leo inasadifiana na Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Quds. Hii ni siku ya kupata nguvu upya taifa madhulumu la Palestina na ni siku ambayo inaunganisha nguvu za umma mzima wa Waislamu na kila mpenda haki duniani katika kupambana na utawala wa kibaguzi wa Kizayuni.
Habari ID: 1433171 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/25
Kiongozi Muadhamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwamba, njia pekee ya kukabiliana na utawala wa kinyama wa Israel, ni kuwepo muqawama wa kutumia silaha wa Wa palestina na kupanuka wigo huo wa mapambano hadi kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 1433169 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/25
Hatimaye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Julai 20 lilivunja kimya chake na kudai kuwa linasikitishwa na idadi kubwa ya raia wanaouliwa na kujeruhiwa huko Ukanda wa Ghaza na kutaka kusimamishwa mara moja kile ilichokitaja kuwa ni uhasama.
Habari ID: 1432292 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/22
Idadi ya Wa palestina waliouawa shahidi katika mashambulizi ya kikatili yaliyofanywa na jeshi vamizi la Israel katika eneo la Shujaiyya huko Ghaza imepindukia watu 100 na zaidi ya 200 wengine kujeruhiwa.
Habari ID: 1431786 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/21
Utawala haramu wa Israel umezidisha jinai zake dhidi ya Wa palestina wasio na ulinzi kwa kuanzisha hujuma ya kijeshi ya nchi kavu katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 1430956 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/19
Utawala haramu wa Israel unaendeleza jinai zake za kinyama katika Ukanda wa Ghaza ambapo mbali na kuwaua shahidi Wa palestina wakiwemo wanawake na watoto pia utawala huo umebomoa misikiti, nyumba, na mahospitali katika eneo hilo la Palestina.
Habari ID: 1429748 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/14
Rais Hassan Rouhani
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema matatizo wanayokumbana nayo Waislamu hivi sasa ni matokeo ya kutoyazingatia mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Habari ID: 1428807 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/13
Rais Hassan Rouhani
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe kwa viongozi wa nchi zote za Kiislamu duniani na kusisitiza kwamba ulimwengu wa Kiislamu unapasa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha unakomesha haraka iwezekanavyo mzingiro wa kidhulma uliowekwa na Wazayuni dhidi ya wananchi wa eneo la Ukanda wa Ghaza
Habari ID: 1428175 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/07/11
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa wito kwa taifa la Palestina kuuhami na kuulinda Msikiti wa Al Aqsa.
Habari ID: 1395102 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/04/14
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imesema itaunga mkono ombi la Palestina kwa Umoja wa Mataifa kujiunga na na mikataba 15 ya kimataifa.
Habari ID: 1390963 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/04/06
Sambamba na majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuendeleza migogoro katika ardhi za Palestina kwa kuushambulia Msikiti wa kihistoria wa al Aqsa, Uri Ariel Waziri wa Makazi wa utawala huo ghasibu ameukoleza zaidi mgogoro huo kwa kuingia ndani ya msikiti mtakatifu wa al Aqswa.
Habari ID: 1388191 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/03/17
Kundi la kutetea haki za binadamu la Palestina limetangaza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umepiga marufuku adhana katika jela zake wanakoshikiliwa maelfu ya Waislamu wa Ki palestina .
Habari ID: 1377228 Tarehe ya kuchapishwa : 2014/02/19