IQNA

Mayahudi Amerika wakosoa sera za Israel dhidi ya Palestina

12:47 - November 07, 2015
Habari ID: 3444264
Mkuu wa kundi kubwa zaidi la Mayuhudi wanaoishi Amerika ya Kaskazini amekosoa sera potofu za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Kuhani Rick Jacobs, Rais wa muungano wa Mayahudi wanaopigania mageuzi ameitaka jamii ya Mayahudi kutofumbia macho jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu. Kadhalika Jacobs amesema kuwa muungano wao utaendelea kupinga na kukosoa sera za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Rais wa muungano wa Mayahudi wanaopigania mageuzi amesema idadi kubwa ya vijana wa Kiyahudi hawaungi mkono sera za chuki na ubaguzi za utawala huo haramu dhidi ya raia ya kigeni wanaoishi Israel, haswa Waarabu na Mayahudi wa Kiethiopia. Zaidi ya Mayahudi laki 5 wanaishi katika vitongoji haramu zaidi ya 120 vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Mashariki mwa Quds Tukufu tokea mwaka wa 1967.

3444235

captcha