kiislamu - Ukurasa 16

IQNA

Spika wa Majlisi ya Iran
Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu ya Iran (Bunge), amesema kuwa leo ulimwengu wa Kiislamu umekuwa na fursa na nafasi kubwa zaidi hivi sasa ikilinganishwa na miongo iliyopita.
Habari ID: 2692012   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/10

Rais Francois Hollande wa Ufaransa amepinga kuweko uhusiano wowote kati ya wafanya mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo Paris na dini ya Kiislamu.
Habari ID: 2692011   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/10

Waliul Amr wa Waislamu kote duniani
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, umoja ni somo kubwa kutoka kwa Mtume wa Mwisho SAW na kwamba hivi sasa ni hitajio la dharura la umma wa Kiislamu.
Habari ID: 2689577   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/09

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu amewataka Waislamu kuwa macho katika kukabiliana na njama za maadui wa ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 2689576   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/09

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema madola ya kibeberu yanaibua migogoro baina ya Waislamu kwa lengo la kutawala ardhi za Kiislamu zenye umuhimu wa kistratijia.
Habari ID: 2684305   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/07

Mkutano wa 28 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza leo mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu na maulamaa wa ulimwengu wa Kiislamu.
Habari ID: 2684304   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/07

TEHRAN-IQNA- Mashindano ya 5 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yamemalizika Jumapili mjini Tehran huku wawakilishi wa Iran na misri wakichukua nafasi za kwanza katika qiraa na hifdhi kwa taratibu.../mh 2671946
Habari ID: 2672141   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/05

Mwenyekiti wa Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu nchini Iran amesema lengo la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu ni kuimarisha itikadi za wanafunzi wa vyuo vikuu katika ulimwengu wa Kiislamu ili kuhuisha umoja wa Waislamu kueneza ustaarabu mpya wa Kiislamu.
Habari ID: 2666237   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/01

Kikao cha 23 kikuu cha Sala nchini Iran kimefunguliwa Jumatano kwa ujumbe wa Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Ahwaz (kusini magharibi mwa Iran).
Habari ID: 2663165   Tarehe ya kuchapishwa : 2015/01/01

Kiongozi mwandamizi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Uganda Sheikh Ductoor Abdul Qadir Sudi Muwaya aliuawa shahidi Alkhamisi iliyopita. Mkuu wa polisi nchini humo ametangaza kuwa uchunguzi wa kina utafanyika kubainisha aliyetekeleza mauaji hayo.
Habari ID: 2646978   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/29

Tehran (IQNA)- Kongamano la kimataifa lenye anuani ya “Umoja wa Kimataifa Kwa Mtazamo wa Qur’ani na Hadithi” linatazamiwa kufanyika Tehran, Ijumaa tarehe pili Januari.
Habari ID: 2626656   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/25

Tumo katika kumbukumbu ya kufariki dunia Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu Muhammad al-Mustafa SAW. Hii leo imepita zaidi ya miaka 1400 tangu mbora huyo wa viumbe aage dunia; lakini jina la mtukufu huyo pamoja na utajo na shakhsia yake kubwa na adhimu na isiyo na mithili ingali inaleta hamasa katika nyoyo.
Habari ID: 2623557   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/20

Kituo cha Kiislamu cha al Azhar nchini Misri kimetoa wito wa kufukuzwa magaidi wote katika nchi za Waislamu.
Habari ID: 2617813   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/12

Mjumbe maalumu wa rais Vladimir Putin wa Russia amekutana na kufanya mazungumzo na katibu mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
Habari ID: 2615883   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/07

Kiongozi wa Jumuiya ya Jamaatud Dawa nchini Pakistna Hafidh Saeed Ahmad ametoa wito wa kuanzishwa 'Umoja wa Mataifa ya Kiislamu' ili kutatua matatizo waliyonayo Waislamu duniani.
Habari ID: 2615835   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/07

Mkutano wa 10 wa Mawaziri wa Habari wa nchi za Kiislamu (ICIM) umefanyika Jumatano hapa mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na Is’haq Jahangiri Makamu wa Kwanza wa Rais na Katibu Mkuu wa OIC.
Habari ID: 2615009   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/12/04

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ege kilichoko katika mji wa Izmir nchini Uturuki amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela, baada ya kumzuia mwanafunzi aliyevaa hijabu ya Kiislamu kuingia darasani.
Habari ID: 2613249   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/30

Imam Khamenei
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kujihisi kuwa na majukumu ya kibinadamu, kuwa na maarifa ya kumjua Mwenyezi Mungu na busuri, ni misingi mikuu ya fikra za kimantiki za jeshi la kujitolea la Basiji.
Habari ID: 2612444   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/28

Kongamano la Kimataifa kuhusiana na Tishio la Makundi ya Kitakfiri na Yenye Kufurutu Ada limeanza leo katika mji mtukufu wa Qum hapa nchini Iran kwa kuhudhuriwa na masheikh na maulamaa kutoka nchi mbalimbali duniani.
Habari ID: 1476323   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/23

Imam Khamenei
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametahadharisha kuhusu njama za adui zenye lengo za kuudhihirisha Uislamu kuwa ni tishio.
Habari ID: 1474768   Tarehe ya kuchapishwa : 2014/11/18