iran - Ukurasa 2

IQNA

IQNA-Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) amezionya Marekani, Israel na mamluki wao wenye mienendo ya kigaidi kama ile ya Daesh kwamba kosa lolote la kimahesabu litakabiliwa na majibu makali na ya kuangamiza.
Habari ID: 3481805    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/15

IQNA-Mamilioni ya watu wa Iran siku ya Jumatano wamejitokeza katika mazishi na shughuli ya kuwaaga mashahidi wa mashambulizi ya kigaidi mjini Tehran na miji mingine ya Iran.
Habari ID: 3481803    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/15

IQNA – Afisa na msomi mmoja wa masuala ya Qur’ani Tukufu nchini Iran amesisitiza umuhimu wa kutumia uwezo na nafasi ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Tehran yanayokuja ili kulitambulisha neno la Wahyi kwa watu wa ulimwengu.
Habari ID: 3481800    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/14

IQNA – Mwanazuoni wa Ki iran i amesema kuwa Qur’ani Tukufu imetangaza wazi kuwa jukumu lake ni kuanzisha ustaarabu mpya, na adui analijua hilo.
Habari ID: 3481799    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/14

IQNA – Mamilioni ya wananchi nchini Iran waliandamana Jumatatu kulaani ghasia za hivi karibuni zilizochochewa na makundi ya kigaidi yanayodaiwa kuungwa mkono na Marekani na utawala wa Kizayuni.
Habari ID: 3481796    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/13

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, amepongeza maandamano ya kitaifa yaliyoonyesha uungaji mkono kwa Jamhuri ya Kiislamu, akisema wingi wa wananchi waliojitokeza “umeandika historia” na kuvuruga njama za maadui waliolenga kuibua misukosuko kupitia vibaraka wao wa ndani.
Habari ID: 3481795    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/13

IQNA – Akizungumzia machafuko yanayodaiwa kuungwa mkono na Israel katika miji ya Iran, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki alisema kuwa malengo ya utawala wa Israel ndani ya Iran hayatoweza kutimia. Hakan Fidan amesisitiza kuwa utawala wa Tel Aviv hautafanikiwa katika njama zake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Habari ID: 3481794    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/12

IQNA – Jumuiya ya Qur’ani ya Iran imelaani vikali machafuko mabaya yaliyotokea hivi karibuni nchini. Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, jumuiya hiyo iliwashukuru vikosi vya ulinzi na usalama kwa juhudi zao za kurejesha utulivu na amani katika jamii.
Habari ID: 3481793    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/12

IQNA-Serikali ya Iran imetangaza siku tatu za maombolezo kwa ajili ya kuwakumbuka waathiriwa, wakiwemo askari wa vikosi vya usalama na wa jeshi la kujitolea, ambao wameuliwa shahidi na magaidi wafanyaji fujo na vurugu wanaoungwa mkono na Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel, waliojaribu kuteka nyara maandamano ya amani ya wananchi ya kulalamikia hali ya uchumi nchini.
Habari ID: 3481792    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/12

IQNA – Mufti Mkuu wa Lebanon, Sheikh Abdul Latif Darian, amesema kuwa uhusiano kati ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni nchini humo ni wa kindugu na wa kuheshimiana.
Habari ID: 3481787    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/11

IQNA – Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kwamba wakuu Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel wanafanya kila wawezalo kuzuia kuundwa kwa umoja miongoni mwa mataifa ya Kiislamu.
Habari ID: 3481786    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/11

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kundi la watu waharibifu Alhamisi usiku mjini Tehran waliharibu mali za umma na za wananchi kwa ajili ya kumfurahisha rais wa Marekani huku akisisitiza kuwa Iran haitalegeza msimamo katika kukabiliana na magenge ya wahalifu.
Habari ID: 3481785    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/10

IQNA – Kamati ya maandalizi ya Maonyesho ya Kimataifa ya Qur’an Tukufu mjini Tehran imetoa mwito kwa umma kushiriki katika kuchagua kauli mbiu ya toleo la 33 la tukio hili kubwa la Qur’an.
Habari ID: 3481780    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/07

IQNA – Kipindi cha 12 cha mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Dawlat al-Tilawa nchini Misri kiligeuka safari ya kiroho na kihisia, ambapo simulizi binafsi ziliungana na sauti za mbinguni, zikazalisha athari ya kina iliyogusa nyoyo za kila msikilizaji.
Habari ID: 3481773    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/06

IQNA – Reza Safdari, qari mashuhuri kutoka mkoa wa Sistan na Baluchestan, kusini mashariki mwa Iran, amejiunga na kundi la wanaofuzu kuingia fainali za mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yanayofanyika nchini Qatar.
Habari ID: 3481768    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/05

IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwamba kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na kusimama pamoja na wananchi “Inshaallah, tutampigisha magoti adui.”
Habari ID: 3481757    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/03

IQNA-Qari kutoka Iran ameshiriki katika usomaji Qur’an Tukufu katika hafla maalum iliyofanyika mjini Kakani, Bosnia na Herzegovina, usiku wa kuamkia Mwaka Mpya.
Habari ID: 3481753    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/02

IQNA-Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu kwa Papa Leo wa XIV, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, akimpongeza kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Nabii Isa (amani iwe juu yake) na kuwadia Mwaka Mpya wa 2026.
Habari ID: 3481715    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/25

IQNA – Katika ujumbe wake kwa viongozi na wafuasi wa Kanisa Katoliki, Mkuu wa Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO), Hujjatul-Islam Mohammad Mehdi Imanipour, ametumai mwaka 2026 utakuwa mwaka uliojaa amani, mapenzi na huruma kwa wafuasi wote wa dini za mbinguni.
Habari ID: 3481713    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/25

IQNA- Mufti Mkuu wa Uganda, Sheikh Shaban Ramadhan Mubajje, amepongeza juhudi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuimarisha mshikamano wa Waislamu.
Habari ID: 3481696    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/22