iqna

IQNA

iran
Wageni walioshiriki katika Kongamano la 37 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu walitoa heshima zao kwa Imam Khomeini (R.A.) kwa kuhudhuria haram ya mwasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3477685    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/02

Haki za Wanawake katika Uislamu
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran anasema tofauti na Iran, nchi za Magharibi zimekuwa zikikiuka haki za binadamu kwa kuwatumia wanawake kama chombo cha mashinikizo dhidi ya mataifa huru.
Habari ID: 3477684    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/02

Watetezi wa Qur'ani
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: Serikali ya Uswidi inatakiwa kujibu matakwa ya wazi kabisa ya Waislamu kwa kuwajibika na kufuata kikamilifu kanuni za kimsingi za haki za binadamu, kwa kuhimiza maadili na kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini tofauti na kuchukua hatua za kivitendo na zenye ufanisi.
Habari ID: 3477679    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/01

Wiki ya Umoja wa Kiislamu
TEHRAN (IQNA)-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, chaguo la kusalimu amri na kufanya mapatano kiudhalili halipo tena mezani na kwamba wale wanaoweka uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni ni kujitumbukiza kizazi.
Habari ID: 3477677    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/01

Wiki ya Umoja wa Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kongamano la 37 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu limeanza leo jijini Tehran kwa hotuba ya Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3477676    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/01

Umoja wa Waislamu
BERLIN (IQNA) - Balozi wa Iran nchini Ujerumani na Sheikhe Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha al-Azhar ncini Misri walikutana mjini Berlin kujadili masuala muhimu yanayoukabili ulimwengu wa Kiislamu na jinsi ya kustawisha umoja na mshikamano kati ya Waislamu.
Habari ID: 3477590    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/12

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo Jumatatu ameonana na wananchi wa mikoa miwili ya "Sistan na Baluchistan" na ule wa "Khorasan Kusini" na kusisitiza kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesimama imara na kwa nia isiyotetereka katika kukakbiliana na adui.
Habari ID: 3477583    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/11

Diplomasia
TEHRAN (IQNA)- Katika kikao na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza nafasi ya Shahidi Jenerali Soleimani katika kuimarisha usalama wa eneo hili mbele ya Uzayuni na ugaidi.
Habari ID: 3477532    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/01

Umoja wa Waislamu
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ulimwengu wa Kiislamu ambao una umoja na mshikamano ndicho kizingiti kikubwa zaidi kwa ubeberu wa dunia.
Habari ID: 3477530    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/01

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA)- Mahakama ya Denmark imeamua kupiga marufuku kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kufuatia taathira mbaya za hatua hizo.
Habari ID: 3477492    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/25

Diplomasia
TEHRAN (IQNA)- Muungano wa kiuchumi wa BRICS wa masoko yanayoibuka duniani umeamua kutoa mialiko ya uanachama kwa mataifa sita.
Habari ID: 3477490    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/24

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran amesema kuwa, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) ni taasisi kubwa zaidi ya kupambana na ugaidi duniani ambayo inafanya mambo makubwa ya kupigiwa mfano ambayo majeshi makubwa duniani yanashindwa kuyafanya.
Habari ID: 3477453    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/18

Diplomasia
NEW YORK (IQNA)- Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa inayolaani shambulio la hivi karibuni la kigaidi katika Haram Takatifu ya Hadhrat Ahmad bin Musa (AS) maarufu kama Shah Cheragh mkoani Fars kusini mwa Iran.
Habari ID: 3477449    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/17

Hujuma ya kigaidi
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Iran Ebrahim Raisi amewaagiza Waziri wa Mambo ya Ndani Ahmad Vahidi na Gavana wa Mkoa wa Fars Mohammad Hadi Imaniyeh wawatambue haraka na kuwaadhibu wahusika wa shambulio la kigaidi katika Haram Takatifu ya Hadhrat Ahmad bin Musa (AS) maarufu kama Shah Cheragh mjini Shiraz kusini mwa Iran.
Habari ID: 3477434    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/14

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja kazi yenye mafanikio na fahari iliyofanywa na Kundi la 86 la Wanamaji wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuzunguka dunia nzima kuwa ni matokeo ya kazi ngumu, nia thabiti, kujiamini, uwezo wa kubuni, maarifa ya hali ya juu ya kijeshi, uongozi bora na "ujasiri na kusimama imara mkabala wa mashaka ya aina mbalimbali."
Habari ID: 3477391    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/06

Turathi za Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Iran imeteua msikiti wake wa Tarikhaneh, ambao ulijengwa takriban miaka 900, kwa ajili ya kuwekwa katika orodha turathi ya Jumuiya ya Kiislamu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (ICESCO).
Habari ID: 3477385    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/05

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ameeleza kuwa, wale wanaochoma moto nakala za Qur’ani Tukufu kwa hakika wanajichoma moto wao wenyewe na kusema: Si jambo rahisi kwa kila mtu kujua hakika ya Qur’ani ambayo ni roho na rehema ya Mwenyezi Mungu, na kufanya ukaidi dhidi ya neno la Mungu ni ishara ya roho ya kishetani.
Habari ID: 3477381    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/04

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hossein Amir Abdollahian amewasilisha mapendekezo ya Iran kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Ulaya.
Habari ID: 3477369    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/01

Watetezi wa Qur'ani Tukufu
TEHRAN (IQNA)- Sheikh wa Al-Azhar wa nchini Misri, akijibu barua ya mkuu wa vyuo vya kidini vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ameeleza matumaini yake kuwa msimamo wa pamoja uliochukuliwa na Waislamu hivi karibuni katika kukabiliana na suala la kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu utakuwa kichocheo cha kutatua tofauti na kuleta umoja baina yao.
Habari ID: 3477367    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/01

Muharram 1435
TEHRAN (IQNA)- Mamilioni ya Waislamu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na maeneo mengine ya dunia leo wameshiriki shughuli ya siku ya Ashura ya kukumbuka siku ya kuuliwa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (AS).
Habari ID: 3477351    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/28