IQNA- Katika harakati inayoashiria istiqama, Wapalestina katika Ukanda wa Gaza siku ya Ijumaa walishiriki katika sala ya kwanza ya Ijumaa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Machi 15 katika eneo lenye mabaki ya Msikiti wa Rafah ambalo ulibomolewa hivi karibuni katika hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3478527 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/17
Kadhia ya Palestina
IQNA-Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Afrika Kusini amesema kuwa, raia yeyote wa nchi hiyo atakayeusaidia utawala wa Kizayuni katika vita vya Ukanda wa Gaza atatiwa mbaroni punde tu atakaporejea Afrika Kusini.
Habari ID: 3478520 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/16
Kadhia ya Palestina
IQNA - Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) amesema nchi za Kiislamu zinapaswa kuunga mkono kikamilifu Afrika Kusini katika kesi yake ya kisheria dhidi ya utawala wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ)
Habari ID: 3478502 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/13
Wapalestina katika Mwezi wa Ramadhani
IQNA - Rais wa Jumuiya ya Wahubiri wa Kiislamu Palestina ametoa wito kwa Waislamu wote wanaofunga mwezi mtukufu wa Ramadhani waombe dua kwa ajili kukomeshwa mateso na masaibu wanayokumbana nao watu wa Gaza.
Habari ID: 3478495 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/12
Ramadhani Palestina
IQNA - Waislamu wa Palestina huko Gaza wamebakia imara katika Imani na hivyo wana azma ya kutekeleza ibada zote za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kukusanyika katika mabaki ya misikiti iliyoharibiwa na mabomu ya utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3478485 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/10
Kadhia ya Palestina
IQNA - Msemaji wa Harakati ya Ansarullah inayotawala Yemen amesisitiza kwamba jambo muhimu zaidi kwa Waislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ni uungaji mkono kwa Wapalestina wanaoteseka huko Gaza.
Habari ID: 3478464 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/07
Kadhia ya Palestina
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepanda mzeituni katika hatua ambayo ameitaja kuwa ni mshikamano na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
Habari ID: 3478453 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/05
Jinai za Israel
IQNA-Viongozi wa dunia wameendelea kulaani kitendo cha wanajeshi wa Israel kuwaua Wapalestina 116 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 760 waliokuwa wakisubiri msaada wa chakula katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa siku ya Alhamisi.
Habari ID: 3478438 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/02
Uchaguzi wa Iran
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema: Maadui wa Iran ya Kiislamu wana hofu ya kushiriki kwa wingi kwa wananchi katika uchaguzi hapa nchini.
Habari ID: 3478428 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/28
Jinai za Israel
IQNA - Brazil imesisitiza haja ya utawala haramu wa Israel kufuata kikamilifu hatua za dharura zilizoamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) mwezi uliopita kuhusu hali ya Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478421 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/27
Jinai za Isarel
IQNA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesikitishwa na mauaji ya utawala haramu wa Israel dhidi ya raia katika Ukanda wa Gaza, akisema hali hiyo inatishia sheria za kimataifa za kibinadamu.
Habari ID: 3478420 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/27
Mapambano ya Kiislamu yaani Muqawama
IQNA - Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (muqawama) ya al-Nujaba ya Iraq amesema harakati hiyo itaendelea kulenga ngome za utawala wa Kizayuni kwa lengo la kuonyesha mshikamano na Palestina.
Habari ID: 3478414 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/26
Watetezi wa Palestina
IQNA-Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimelaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza, na kuonya kuhusu maafa ya binadamu katika eneo hilo.
Habari ID: 3478350 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/14
Jinai za Israel
IQNA-Utawala katili wa Israel umeendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kwa kutekeleza mashambulizi makubwa ya anga na mizinga katika mji wa Rafah kusini mwa ukanda huo na kuua na kujeruhi mamia ya raia wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Habari ID: 3478339 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/12
Jinai za Israel
IQNA - Msichana wa Kipalestina mwenye umri wa miaka sita, ambaye alikuwa ametoweka kwa wiki mbili baada ya gari la familia yake kufyatuliwa risasi na wanajeshi katili wa utawala haramu wa Israel, alipatikana amekufa.
Habari ID: 3478327 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/10
Jinai za Israel
IQNA-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limeonya kwamba mashambulizi ya utawala haramu wa Israel dhidi ya mji wa mpakani wa Rafah wenye msongamano mkubwa wa watu Gaza yatakuwa "kichocheo cha maafa."
Habari ID: 3478326 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/09
Ulimwengu wa Kiislamu
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumza kuhusu tukio chungu na la kuhuzunisha la Gaza na kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni, na akasema: “masaibu ya Gaza ni masaibu ya wanadamu na yanaonyesha kuwa utaratibu wa sasa wa ulimwengu ni wa batili tupu, usioweza kudumu na utatoweka tu.
Habari ID: 3478321 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/08
Wanajihadi
IQNA - Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utapanua mashambulizi yake dhidi ya Lebanon, utapata jibu kali na la sawasaw kutoka kwa harakati hiyo.
Habari ID: 3478261 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/27
Al Houthi
IQNA-Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen Abdul-Malik al-Houthi anasema kulengwa kwa meli zinazohusishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel kutaendelea katika Bahari ya Sham hadi Wapalestina walioko Gaza watakapoweza kupokea misaada.
Habari ID: 3478254 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/26
Harakati za Qur'ani
IQNA - Kijana wa Kipalestina amezindua mpango wa kusambaza nakala za Qur’ani Tukufu miongoni mwa wale wanaoishi katika kambi za wakimbizi katika eneo la Gaza ambalo linakabiliwa na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3478253 Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/25