iqna

IQNA

Jinai za Israel
IQNA-Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, Hamas, amethibitisha habari ya kuuawa shahidi watoto na wajukuu zake katika shambulio la kinyama la utawala wa Kizayuni na akasema: "kwa machungu haya na kwa damu hii tunajenga matumaini, mustakbali na uhuru wa watu wetu, piganio letu na taifa letu".
Habari ID: 3478669    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/11

Kadhia ya Gaza
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Ghaza ni suala ambalo haliwezi kufumbiwa macho kwani ndiyo kadhia kuu ya Ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa, hivyo kila mmoja wetu anapaswa kutekeleza vizuri majukumu yake kuhusu Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3478666    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/10

Sikukuu ya Idul Fitr
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei anasema utawala wa Kizayuni wa Israel "lazima uadhibiwe na kutiwa adabu" kwa shambulio lake baya dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
Habari ID: 3478662    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/10

Qur'ani na Palestina
IQNA - Programu khitma ya Qur'ani zilifanyika Jumatatu katika shule zaidi ya 20,000 nchini Iran na nchi kadhaa duaniani kuwakumbuka mashahidi mabarobaro Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478660    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/09

Mtazamo
IQNA - Imamu mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri alisema matukio machungu yanayotokea duniani yanadhihirisha ukweli kwamba ubinadamu unahitaji mafundisho ya Qur'ani Tukufu.
Habari ID: 3478645    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/04/07

Siku ya Quds
IQNA - Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyed Hasan Nasrallah ametoa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi barabarani Ijumaa ijayo ambayo inaadhimishwa kama Siku ya Kimataifa ya Quds.
Habari ID: 3478605    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/30

Waislamu na kadhia ya Gaza
IQNA - Katika Amerika ya Kusini, jamii za Waislamu zinaadhimisha Ramadhani mwaka huu bila mazingira ya sherehe ambayo ni ya kawaida wakati wa mlo wa futari kutokana na mateso huko Gaza, ambapo zaidi ya Wapalestina 32,500 wameuawa tangu utawala wa Israel uanzishe vita eneo hilo Oktoba 7.
Habari ID: 3478603    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/30

Diplomasia ya Kiislamu
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, Muqawama (mapambano ya Kiislamu) usio na kifani wa vikosi vya Muqawama na watu wa Ghaza umeutukuza Uislamu.
Habari ID: 3478588    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/27

Waislamu Uingereza
IQNA - Ufafanuzi wa hivi majuzi wa itikadi kali uliopendekezwa na serikali ya Uingereza umelaaniwa kwa kuwalenga Waislamu nchini humo.
Habari ID: 3478568    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/24

IQNA- Katika harakati inayoashiria istiqama, Wapalestina katika Ukanda wa Gaza siku ya Ijumaa walishiriki katika sala ya kwanza ya Ijumaa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Machi 15 katika eneo lenye mabaki ya Msikiti wa Rafah ambalo ulibomolewa hivi karibuni katika hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3478527    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/17

Kadhia ya Palestina
IQNA-Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Afrika Kusini amesema kuwa, raia yeyote wa nchi hiyo atakayeusaidia utawala wa Kizayuni katika vita vya Ukanda wa Gaza atatiwa mbaroni punde tu atakaporejea Afrika Kusini.
Habari ID: 3478520    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/16

Kadhia ya Palestina
IQNA - Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) amesema nchi za Kiislamu zinapaswa kuunga mkono kikamilifu Afrika Kusini katika kesi yake ya kisheria dhidi ya utawala wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ)
Habari ID: 3478502    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/13

Wapalestina katika Mwezi wa Ramadhani
IQNA - Rais wa Jumuiya ya Wahubiri wa Kiislamu Palestina ametoa wito kwa Waislamu wote wanaofunga mwezi mtukufu wa Ramadhani waombe dua kwa ajili kukomeshwa mateso na masaibu wanayokumbana nao watu wa Gaza.
Habari ID: 3478495    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/12

Ramadhani Palestina
IQNA - Waislamu wa Palestina huko Gaza wamebakia imara katika Imani na hivyo wana azma ya kutekeleza ibada zote za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kukusanyika katika mabaki ya misikiti iliyoharibiwa na mabomu ya utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3478485    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/10

Kadhia ya Palestina
IQNA - Msemaji wa Harakati ya Ansarullah inayotawala Yemen amesisitiza kwamba jambo muhimu zaidi kwa Waislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ni uungaji mkono kwa Wapalestina wanaoteseka huko Gaza.
Habari ID: 3478464    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/07

Kadhia ya Palestina
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepanda mzeituni katika hatua ambayo ameitaja kuwa ni mshikamano na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
Habari ID: 3478453    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/05

Jinai za Israel
IQNA-Viongozi wa dunia wameendelea kulaani kitendo cha wanajeshi wa Israel kuwaua Wapalestina 116 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 760 waliokuwa wakisubiri msaada wa chakula katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa siku ya Alhamisi.
Habari ID: 3478438    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/02

Uchaguzi wa Iran
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema: Maadui wa Iran ya Kiislamu wana hofu ya kushiriki kwa wingi kwa wananchi katika uchaguzi hapa nchini.
Habari ID: 3478428    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/28

Jinai za Israel
IQNA - Brazil imesisitiza haja ya utawala haramu wa Israel kufuata kikamilifu hatua za dharura zilizoamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) mwezi uliopita kuhusu hali ya Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478421    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/27

Jinai za Isarel
IQNA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesikitishwa na mauaji ya utawala haramu wa Israel dhidi ya raia katika Ukanda wa Gaza, akisema hali hiyo inatishia sheria za kimataifa za kibinadamu.
Habari ID: 3478420    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/27