iqna

IQNA

Waungaji mkono Palestina
TEHRAN (IQNA)- Katika muendelezo wa himaya na uungaji mkono wa ulimwengu kwa mapambano ya wananchi wa Gaza na kulaani jinai za utawala ghasibu wa Israel, maelfu ya wananchi wa Pakistan wameandamana na kuelekea katika ubalozi mdogo wa Marekani.
Habari ID: 3477967    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/30

Kimbunga cha Al Aqsa
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei anasema tukio la kihistoria la Kimbunga cha al-Aqsa cha harakati ya Hamas kimsingi lilikuwa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, lakini limeweza kuvuruga sera za Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia na litaifuta kabisa ajenda hiyo.
Habari ID: 3477965    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/29

Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA)- Kutokana na udharura na haja ya kuongezwa na kuimarishwa umoja na mshikamano baina ya wapenda uhuru na wapigania haki hususan nchi za Kiislamu katika kuilaani Israel, Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Mahathir Mohammad amesema: “Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, ili nchi za Kiislamu zimshinde Mzayuni na adui wao wa pamoja hazina njia nyingine ghairi ya kudumisha umoja, kuimarisha msingi wa ulinzi na nguvu za kijeshi.
Habari ID: 3477964    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/29

Jinai za Israel
Jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel limekiri kuwa zaidi ya askari wake 1,000 wa walowezi wa utawala huo waliuawa wakati wa mapigano ya Kimbunga cha Al-Aqsa.
Habari ID: 3477959    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/28

Waislamu Ujerumani
BERLIN (IQNA) – Kiongozi mmoja wa jamii ya Waislamu nchini Ujerumani ameelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya Waislamu nchini humo kufuatia vita vya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza.
Habari ID: 3477958    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/28

Jinai Marekani
VERMONT (IQNA) - Polisi wa Jimbo la Vermont waliripoti Jumapili kwamba vijana watatu wa Kipalestina walipigwa risasi na kujeruhiwa karibu na Chuo Kikuu cha Vermont.
Habari ID: 3477954    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/27

Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, Harakati ya Kiislamu (Muqawama) ya Kupigania Ukombozi wa Palestina (HAMAS) ilivunja mgongo wa Israel kwa kutegemea imani na ushujaa katika operesheni ya kimbunga ya Al-Aqswa.
Habari ID: 3477938    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/24

Watetezi wa Palestina
TUNIS (IQNA) - Rached Ghannouchi, mkuu wa Chama cha Ennahda cha Tunisia, alielezea Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa kama zawadi kwa Umma wa Kiislamu.
Habari ID: 3477934    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/23

Mapambano dhidi ya Israel
SANAA (IQNA) - Yemen imevurumisha makombora ya cruise dhidi ya maeneo ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel
Habari ID: 3477933    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/23

Harakati za Mapambano ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah jana Jumatano alikutana na ujumbe wa maafisa wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS mjini Beirut kujadili matukio ya Gaza, huku idadi ya wananchi wa Palestina waliouawa shahidi kwenye mashambulizi ya kikatili ya Israel katika eneo hilo linalokaliwa kwa mabavu ikikaribia 15,000.
Habari ID: 3477931    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/23

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amesema utawala haramu wa Israel "iliangushwa" katika Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, operesheni kubwa zaidi ya kijeshi kuwahi kufanywa na makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina dhidi ya utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3477929    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/22

Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA)- Hatimaye kumefikiwa makubaliano ya kusitisha vita huko Gaza kwa muda wa siku nne ili kutoa fursa ya kufikishwa misaada ya kibinadamu na pande mbili kubadilishana mateka.
Habari ID: 3477928    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/22

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Mwanaharakati wa Gaza na mkuu wa shirika la kutoa misaada anasema Wapalestina hawawezi tena kuamini sheria za kimataifa kwani zimeshindwa kuwalinda watoto ambao wanakabiliwa na uvamizi wa kikatili wa Israel.
Habari ID: 3477926    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/21

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) – Zaidi ya watoto 5,000 wameuawa katika vita vya mauaji ya kimbari vya utawala katili wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7. Onyo: Video hii ina matukio ambayo wengine wanaweza kupata ya kuwasumbua.
Habari ID: 3477925    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/21

KUALA LUMPUR (IQNA) – Mkutano ulifanyika katika Msikiti wa Sultan Iskandar ulioko Bandar Dato' Onn huko Johor, Malaysia, Jumapili jioni kwa ajili ya mshikamano na watu wa Palestina.
Habari ID: 3477920    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/20

Diplomasia ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi amewaandikia barua wakuu na viongozi wa nchi 50 duniani kuwahimiza kuwa na kauli moja kuhusu wajibu wa kukomeshwa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Gaza.
Habari ID: 3477919    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/20

Watetezi wa Palestina
CANBERRA (IQNA) – Maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina waliandamana kote Australia wikiendi hii, wakitoa wito wa kukomeshwa mara moja kwa mashambulizi ya kinyama ya utawala haramu wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza ambayo yameua zaidi ya watu 13,000, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, tangu Oktoba 7.
Habari ID: 3477918    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/20

Jinai za Israel
RABAT (IQNA) - Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi, na Utamaduni (ISESCO) limetoa tamko kali siku ya likilaani mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya shule mbili kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kuwa ni "fedheha kwa ubinadamu" na "uhalifu wa kutisha".
Habari ID: 3477917    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/20

Watetezi wa Wapalestina
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: kadhia za Gaza zimewadhihirishia walimwengu hakika nyingi zilizofichika, na moja wapo ya hakika hizo ni uungaji mkono wa viongozi wa nchi za Magharibi kwa ubaguzi wa rangi.
Habari ID: 3477916    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/19

Watetezi wa Palestina
TEHRAN (IQNA)- Watu wa Iran ya Kiislamu jana Jumamosi walishiriki katika maandamano makubwa kote nchini kuwatetea watoto wanaoendelea kuuawa wa Palestina sambamba na kulaani "mauaji ya watoto wachanga", "uhalifu", "mauaji ya kimbari", "mauaji ya halaiki", "ugaidi", "uhalifu wa kivita" na "maafa ya binadamu" yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3477915    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/19