iqna

IQNA

Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) - Mashambulio yasiyokoma ya utawala haramu wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza yaliyoanza tarehe 7 Oktoba yamesababisha hospitali 22 na karibu vituo 50 vya afya katika eneo la pwani kuacha kutoa huduma.
Habari ID: 3477885    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/13

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina, kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala wa Kizayuni huko Gaza, kwa wastani, mtoto wa Kipalestina huuawa shahidi kila baada ya dakika 10 katika eneo hilo.
Habari ID: 3477880    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/12

Waungaji mkono Palestina
CAPE TOWN (IQNA) – Mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini ulishuhudia maandamano makubwa zaidi katika jiji hilo katika miaka kadhaa wakati makumi ya maelfu ya watu walikusanyika kutan gaza mshikamano na Palestina, wakitaka kukomeshwa kwa ukatili wa Israel huko Gaza.
Habari ID: 3477879    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/12

Diplomasia ya Kiislamu
RIYADH (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika kikao cha pamoja cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwamba: kadhia ya Gaza ni makabiliano baina ya mhimili wa sharafu au heshima na mhimili wa uovu, na kila mtu anapaswa abainishe yuko upande gani.
Habari ID: 3477878    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/11

Diplomasia ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kikao cha wakuu wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kilichofanyika mjini Riyadh, Saudi Arabia kimetilia mkazo ulazima wa kuondolewa mzingiro dhidi ya Gaza na kuingia misafara ya misaada ya kibinadamu katika eneo hilo.
Habari ID: 3477877    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/11

Jinai za Israel
GAZA (IQNA)- Kuendelea mashambulizi ya kila upande ya jeshi la Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza na kujiri mapigano makali kati ya vikosi vya muqawama na wavamizi hao karibu na kambi ya al-Shati iliyoko magharibi mwa mji wa Gaza, ni baadhi ya habari za hivi karibuni kutoka Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
Habari ID: 3477873    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/10

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)-Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina amewasilisha faili mbele ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kulalamikia matamshi ya vitisho ya waziri wa utawala wa Kizayuni kwamba ikilazimu, utawala huo haramu utatumia bomu la nyuklia dhidi ya watu wa Gaza.
Habari ID: 3477870    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/10

Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA) - Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, nchi zinazoinukia kiuchumi na nchi zinazoendelea zina uwezo mkubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika kuchangia msingi wa mfumo mpya wa dunia.
Habari ID: 3477868    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/10

Jinai za Israel
PRETORIA (IQNA)-Afrika Kusini imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake makuu mjini The Hague (ICC) kuuwajibisha utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na vitendo vyake vya ukiukaji wa sheria za kimataifa wakati utawala huo ukiendelea kufanya jinai dhidi ya binadamu katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3477867    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/09

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Mwandishi mwingine wa habari wa Kipalestina ameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza huku vita vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza vikiendelea kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja.
Habari ID: 3477860    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/08

Kimbunga cha Al Aqsa
BEIRUT (IQNA) - Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) ya Hizbullah ya Lebanon amesema Operesheni ya Kimbunge cha al-Aqsa kama kielelezo cha ujasiri, na uchamungu waa watu wa Palestina.
Habari ID: 3477859    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/08

Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) – Utawala wa Kizayuni wa Israel hadi sasa umeshambulia na kuharibu kabisa kwa mabomu misikiti 56 tokea unazish vita vya maangamizi ya umati dhidi ya Ukanda wa Gaza. Aidha misikiti mingine zaidi ya 192 imepata hasara kwa kuharibiwa katika mashambulizi hayo ya kinyama.
Habari ID: 3477855    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/07

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema machaguo yote dhidi ya utawala haramu wa Israel yapo mezani, huku akiuasa utawala huo wa Kizayuni usitishe mara moja uvamizi na mashambulizi yake ya kinyama dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3477836    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/03

Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA)- Akizungumza leo katika sala ya Ijumaa ya mjini Tehran, Hujjatul Islam wal Muslimeen Kazem Sediqi amesema kuwa leo mrengo wa mapambano ya Kiislamu ni mrengo wa kimataifa na kuongeza kwamba mrengo huo umabadilisha dunia.
Habari ID: 3477832    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/03

Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Ali Barka, mmoja wa viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiisalmu ya Palestina, ,Hamas , nje ya nchi amesema kuwa, utawala haramu wa Israel unawaangamiza Wapalestina kwa umati kwa mabomu ya kisasa ya Marekani.
Habari ID: 3477829    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/02

Jinai za Israel
GENEVA (IQNA) - Kamati ya haki za watoto ya Umoja wa Mataifa imeonya kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya watoto katika vita vinavyoendelea vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Gaza, ikilaani vikali mauaji yanayotekelezwa na utawala huo dhidi watoto katika vita hivyo vya kikatili.
Habari ID: 3477828    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/02

Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) - Idadi ya misikiti iliyoharibiwa kabisa katika mashambulizi yanayoendelea ya utawala haramu wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza imefikia 52.
Habari ID: 3477827    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/02

Kadhia ya Palestina
SANTIAGO (IQNA) - Baada ya Bolivia kukata uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel, nchi nyingine mbili za Amerika ya Latini zimewataka mabalizo wao walioko Israel kurejea nyumbani.
Habari ID: 3477826    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/01

Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA)- Katika kueleza mafanikio ya subira na kusimama kidete Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Watu wa Ghaza wameamsha dhamiri ya mwanadamu kwa subira yao.
Habari ID: 3477822    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/01

Kimbunga cha Al Aqsa
CAIRO (IQNA) – Sheikhe mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri amesifu ushujaa na ujasiri wa watu wa Ukanda wa Gaza katika kukabiliana na mashambulizi makali ya Israel.
Habari ID: 3477821    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/31