iqna

IQNA

Mwanaharakati wa Kuwait
IQNA - Mwanaharakati mmoja wa Kuwait alielezea hali ya sasa ya Palestina na vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ghaza kuwa ni fedheha kwa nchi zinazodai kuwa watetezi wa haki za binadamu.
Habari ID: 3478223    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/20

Watetezi wa Palestina
IQNA – Watu nchini Bahrain wameshiriki maandamano kueleza mshikamano wao na watu wa Palestina na wapiganaji wa Yemen.
Habari ID: 3478220    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/20

Jinai za Israel
IQNA - Shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu (OCHA) liliripoti kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umeendelea kuzuia utoaji wa misaada muhimu ya kibinaadamu ikiwa ni pamoja na dawa muhimu na mafuta ya kuendesha huduma za maji na usafi wa mazingira kaskazini mwa Gaza.
Habari ID: 3478204    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/16

Kiongozi wa Hizbullah
IQNA-Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesema utawala haramu wa Israel mepata hasara "isiyo na kifani" mikononi mwa makundi ya Kiiislamu ya kupigania ukombozi wa Palestina (muqawama) na imeshindwa kufikia malengo yake yoyote baada ya siku 100 za vita vyake vya mauaji ya kimbari kwenye Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478199    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/15

Watetezi wa Palestina
IQNA - Mashirika kadhaa ya Kiislamu nchini Kanada (Canada) yamemuomba Waziri Mkuu Justin Trudeau kuunga mkono uchunguzi wa kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita wa utawala wa Israel huko Gaza.
Habari ID: 3478177    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/10

Chuki dhidi ya Uislamu
IQNA – Vita vya utawala haramu wa Israeli dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza vimezidisha hisia dhidi ya Uislamu duniani (Islamophobia) kote, anasema mwanachama wa kundi kubwa zaidi la kutetea haki za Waislamu nchini Marekani.
Habari ID: 3478172    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/09

Jinai za Israel
IQNA-Mashtaka ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kuhusu tuhuma za mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza kuanza kusikilizwa wiki ijayo.
Habari ID: 3478147    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/04

Kadhia ya Palestina.
IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amesema mpaka wa ulimwengu wa Kiislamu uko Gaza hivi leo, na kwamba Wapalestina wa eneo hilo wamesimama dhidi ya kiburi au mfumo wa kiistikbari na Marekani.
Habari ID: 3478140    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/03

Jinai za Israel
IQNA - Zaidi ya maeneo 200 ya kiakiolojia na ya kale katika Ukanda wa Gaza yameharibiwa na uvamizi wa kijeshi wa Israel tangu Oktoba 7, kulingana na mamlaka huko Gaza.
Habari ID: 3478117    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/31

Waislamu Marekani
IQNA - Baadhi ya viongozi wa Kiislamu wa Marekani wanaripotiwa kusita kufanya kazi na Ikulu ya White House katika kuandaa mkakati wa kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) kutokana na utawala wa Rais Joe Biden kuendelea kuunga mkono vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza.
Habari ID: 3478109    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/29

Watetezi wa Palestina
IQNA - Waandamanaji kutoka matabaka mbalimbali walifanya maandamano mjini The Hague, Uholanzi kudai haki kwa Wapalestina na uchunguzi wa jinai zinazofanywa na utawala wa Israel huko Gaza.
Habari ID: 3478106    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/28

IQNA-Rais Miguel Diaz-Canel wa Cuba amelaani vikali mauaji ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kueleza kwamba, mauaji hayo ya kimbari ni kashfa na fedheha kwa ubinadamu.
Habari ID: 3478104    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/28

Watetezi wa Palestina
IQNA - Mikutano ya hadhara imefanyika katika miji katika nchi mbalimbali za Magharibi mwishoni mwa juma kupinga mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza na kutaka kuwasilishwa kwa misaada ya kibinadamu katika eneo lililozingirwa.
Habari ID: 3478086    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/24

Kadhia ya Palestina
IQNA-Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hatimaye limepitisha azimio kuhusu jinai za Israel dhidi ya Gaza, likidai kuongezwa kwa misaada katika eneo lililozingirwa lakini lakini limeshindwa kuulazimisha utawala haramu wa Israel usitishe vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika eneo hilo.
Habari ID: 3478078    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/23

Watetezi wa Palestina
IQNA - Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Ansarullah nchini Yemen imetan gaza kuanza mchakato wa uhamasishaji wa vijana wanaojitolea kuenda kupigana katika vita vya Gaza pamoja na wapiganaji wa harakati za Kiislamu huko Palestina.
Habari ID: 3478070    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/21

Mapambano ya Wapalestina
IQNA - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Muqawama) ya Palestina, Hamas, Ismail Haniya amesisitiza uthabiti na azma la harakati hiyo katika kuendeleza mapambano ya kupigania ukombozi wa Palestina.
Habari ID: 3478066    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/20

IQNA Ripoti ya kutisha iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Palestina, imefichuliwa kuwa wakati wa hujuma za hivi karibuni za kijeshi za utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza, asilimia 70 ya watu 18,800 waliouawa walikuwa wanawake na watoto.
Habari ID: 3478053    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/18

Watetezi wa Palestina
IQNA - Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kiislamu yenye makao yake London (IHRC) amekosoa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa undumilakuwili wake linapokuja suala la kushtaki wahusika wa uhalifu wa kivita.
Habari ID: 3478050    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/17

Watetezi wa Palestina
IQNA – Toleo la 19 la Jukwaa la Kimataifa la Russia na Ulimwengu wa Kiislamu lilifanyika mjini Moscow huku wazungumzaji wakizingatia hali mbaya ya Gaza.
Habari ID: 3478028    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/13

Matukio ya Palestina
IQNA- Idara ya Habari ya Serikali ya Gaza imeripoti kwamba asilimia 61 ya nyyumba za raia wa Kipalestina huko Ukanda wa Gaza zimebomolewa katika vita vya maangamizi ya umati vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo lilolozingirwa.
Habari ID: 3478026    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/12/12