IQNA

Waislamu milioni 3 katika Ibada ya Hija

12:45 - October 03, 2014
Habari ID: 1456586
Mahujaji takribani milioni tatu wa Nyumba Tukufu ya Allah SWT leo Ijumaa wameanza kutekeleza ibada ya Hijja, ambapo jana usiku walianza kukusanyika katika viwanja vya Arafa nje ya mji mtukufu wa Makka.

Mahujaji watatumia siku nzima ya leo Ijumaa katika eneo hilo tukufu kufanya ibada na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Idul Adh'ha inatarajiwa kusherehekewa siku ya Jumamosi nchini Saudi Arabia ambapo Mahujaji wataendelea kutekeleza ibada hiyo katika uwanja wa Mina kwa kumpiga mawe shetani, kuchinja na kunyoa vichwa vyao katika siku ya kwanza ya Iddi. Baada ya hapo Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu wataelekea Makka kufanya twawafu na kukimbia baina ya Swafa na Marwa.

Ibada ya Hijja inafanyika huku serikali ya Saudi Arabia ikichukua tahadhari kubwa kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kwa kuwachunguza na kuwapima mahujaji hasa wanaotoka kwenye maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo.../mh

1456548

 

Kishikizo: hija arafa waislamu
captcha