IQNA

Hija katika Uislamu /4

Hija: Safari ya Mapenzi

15:24 - November 05, 2023
Habari ID: 3477844
TEHRAN (IQNA) – Hija ni safari ya upendo, ni safari ya mapenzi ya mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu. Hii ndio sababu waja wengi wema wa Mwenyezi Mungu hupendelea kuenda kwa miguu hadi katika mji mtakatifu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija.

Imam Kadhim (AS) alikwenda Makkah kwa ajili ya kuhiji kwa miguu mara kadhaa.

Hija imekuwa rejeleo la zama zote. Hata karne nyingi kabla ya ujio wa Uislamu na hata Uyahudi, Nabii Shuaib (AS) alimwambia Musa (AS) kwamba atamwoza binti yake mmoja kwa sharti kwamba Musa (AS) amsaidie Hija nane. Alitumia Hija nane badala ya miaka minane.

Kuhiji ni sawa na kutafakari kuhusu Qur'ani Tukufu kwani mtu hujifunza mambo mapya kila wakati.

Hija sio safari ambayo kina chake kinaweza kufahamika kupitia vitabu, karatasi, mashairi n.k.

Mtu fulani alimwambia Imam Ali (AS) kwamba kila mara anasikia mambo mapya kutoka kwake kuhusu Hija kwa miaka mingi. Imam akajibu: Je, unatarajia siri za Hija kuwa na mwisho?

Hakuna serikali duniani, hata iwe tajiri na yenye nguvu kiasi gani, ambayo inaweza kuwafanya watu wengi sana kutoka sehemu mbalimbali za dunia kufunga safari kama ya Hija kwa  kwa shauku na motisha ya hali ya juu.

Si tu kuwa Waislamu wanahimizwa kwenda Hija bali matajiri pia matajiri katika jamii  wanahimizwa kuwasaidia wengine kutimiza faradhi hii muhimu ya Hija.

Hija  ni safari ya kwenda Makka ambako kuna Ka’aba Tukufu. Ili kutambua utakatifu wa Ka’aba, inatosha kujua kwamba kila kitu kuanzia kuchinja mnyama hadi kuweka maiti kaburini kinapaswa kufanywa kwa kuelekea katika Ka’aba.

Kaaba ni tukufu kiasia kwamba kupigana vita karibu nayo ni marufuku.

Ni eneo takatifu sana kiasi kwamba kwamba Ibrahim (AS) na Ismail (AS) walikuwa watumishi wa eneo hilo na hakuna yeyote isipokuwa wachamungu ndio wanaostahiki kuwa walinzi wa eneo hili tukufu.

NI eneto takatifu sana kiasi  kwamba Imam Sadiq (AS) alishuka kwenye ngamia karibu na Makka na kutembea sehemu iliyobakia bila viatu.

Ni eneo takatifu kiasi kwamba yeyote atakayekutana kwa wema na wale wanaokwenda Hija, atakapfika nyumba atapata baraka tele za Mwenyezi Mungu.

Baada ya Salah na Zakat, tunaweza kusema kuwa Hija ndiyo amali yenye  aya nyingi za Qur'ani Tukufu zinazoihusu.

Hivyo Hija hii isichukuliwe kirahisi.

Katika Hadith, Mahujaji wanasisitizwa kuwafahamisha wengine kuhusu safari hiyo kabla ya kuifanya na kuleta zawadi na ukumbusho wanaporudi.

Itakuwa ni masikitiko na majuto ikiwa safari hii ya kimungu itadhoofishwa na nia potovu au malengo madogo. Kwa mujibu wa 

Itakuwa ni masikitiko na majuto ikiwa safari hii ya kimungu itadhoofishwa na nia potovu au malengo madogo. Kwa mujibu wa Hadith, katika zama za kukaribia mwisho wa dunia, wafalme wataenda Makka kwa ajili ya burudani, wafanyabiashara kwa ajili ya kupata pesa, wahitaji kwa ajili ya kuomba, na wasomaji wa Qur'an kwa ajili ya kujionyesha au riaa.

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hija uislamu
captcha