IQNA

Marekani inatumia Daesh (ISIS) kuligawa eneo la Mashariki ya Kati

18:33 - August 15, 2015
Habari ID: 3344476
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Marekani inalitumia kundi la kigaidi la Daesh kuligawa eneo la Mashariki ya Kati.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa Washington na waitifaki wake wanatumia ugaidi hususan kundi la kigaidi la Daesh kama wenzo wa kutekeleza njama za kuligawa vipande vipande eneo la Mashariki ya Kati, kuanzia Iraq hadi Syria na hata Saudi Arabia kwa sababu mpango huo unafanyika kwa maslahi ya Marekani na utawala wa Kizayuni.

Ameyasema hayo Ijumaa Alasiri kusini mwa Lebanon kwa mnasaba wa kuadhimisha ushindi wa Hizbullah dhidi ya utawala haramu wa Israel katika vita vya mwaka 2006.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa upo udharura wa kupinga na kukabiliana na mpango wa kuligawa eneo hili. Amesema njama ya kuigawa upya Mashariki ya Kati itasababisha vita vya ndani na vya kikaumu vya muda mrefu, ambavyo matokeo yake yatakuwa uharibifu, maafa na kuongezeka idadi ya wakimbizi.../mh

3342989

captcha