IQNA

Umoja wa Mataifa walaumiwa kunyamazia kimya ukatili wa Saudia nchini Yemen

6:46 - August 29, 2015
Habari ID: 3353340
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ameelezea masikitiko yake kuhusu kimya cha Umoja wa Mataifa na taasisi zingine za kimataifa kuhusu mauaji yanayoendelea dhidi ya watu wasio na hatia nchini Yemen.

Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiqui, Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ameashiria kuendelea hujuma za jeshi la utawala wa Saudi Arabia dhidi ya Yemen na kuuawa Wayemeni wasio na hatia katika uvamizi huo na kuongeza kuwa, 'taifa la Yemen kwa miezi kadhaa sasa limekabiliwa na hujuma isiyo na huruma ya jeshi la Saudi Arabia.' Hujjatul Islam wal Muslimin Siddiqui pia ameashiria kuendelea ukatili wa utawala wa Aal Khalifa dhidi ya watu wa Bahrain na kusema, Wabahrain wanahujumiwa na jeshi la nchi hiyo katika hali ambayo kile wanachotaka ni kupata haki ya kuainisha mustakabali wao. Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ameonya kuwa, kwa kuzingatia hali ya hivi sasa katika eneo la Mashariki ya Kati, Marekani na waitifaki wake wanataka kuzigawa vipande vipande Iraq, Syria na Yemen. Akiashiria msimu unaokaribia wa Hija, Khatibu wa Sala ya Ijumaa amesema, Hija ni kugura na kukata mafungamano na mambo ya kidunia. Katika sehemu nyengine ya hotuba yake Sheikh Siddiqui amesema, kadhia ya Palestina ndio kadhia muhimu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu. Aidha ametoa wito wa kufahamishwa mahujaji mwaka huu kuhusu matatizo yatokanayo na kundi la kigaidi la Daesh au ISIS na Uislamu wa Kimarekani. Halikadhalika ametoa wito wa kuenezwa mafundisho halisi ya Uislamu wenye ukarimu. Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran apia amesema ibada ya Hija inapasa kutumiwa kuimarisha zaidi umoja wa Kiislamu..../mh

3353249

captcha