IQNA

Shehe Mkuu wa Ahul Sunna, Dar es Salaam, Tanzania

Kumbukumbu ya Ashura ni katika nembo za Allah

15:02 - October 15, 2016
Habari ID: 3470614
Sheikh Mussa Salim Al Hadi , Shehe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Tanzania amehutubu katika hadhara ya Mashia na kusema Imam Hussein AS ni wa Waislamu wote duniani na kuadhimisha Ashura ni katika dhihiriso la nembo za Allah.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, nchini Tanzania kumefanyika halfa kubwa za Taasua (Tisa Muharram) na Ashura (10 Muharram) katika kukumbuka kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW, Imam Hussein AS na wafuasi wake 72 watiifu katika jangwa la Karbala. Maelfu ya Waislamu walishiriki katika maombolezo hayo.

Moja ya hafla hizo ni ile iliyofanyika katika Madrassah ya Al Hudaa ambapo mwambata wa utamaduni wa Iran nchini Tanzania Ali Baqeri alihutubu na kusema Imam Hussein AS alikuwa shujaa ambaye hadi lahadha ya mwisho alipipamana kwa ajili ya Tauhidi na kumuabudu Mwenyezi Mungu. Aidha mjini Dar es Salaam kulifanyia matembezi (masir) katika siku ya Taasua ambayo yaliwashirikisha watu wa matabaka mbali mbali katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi hadi katika Msikiti wa Jamia ywa Khoja Shia Ithnaashari. Viongozi wa Kishia na Kisunni walishiriki katika mjumuiko huo akiwemo Shehe Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Mussa Salim Al Hadi. Kumbukumbu ya Ashura ni katika nembo za Allah

Akihutubu katika kikao hicho, Sheikh Hadi alisema: 'Ashura ni kati ya Siku za Allah na ni siku ya huzunu kwa Waislamu na Uislamu. Ashura haina madhehebu maalumu na ni ya Waislamu wote." Aidha aliashiria nafasi maalumu ya Bibi Fatima Zahra SA na Imam Ali AS mbele ya Mtume SAW na kusema: "Hussein AS alikuwa mjukuu wa Mtume SAW na aliuawa shahidi kidhalimu huko Karbala." Sheikh al Hadi amekumbusha kuwa Mtume SAW alisema: "Mwenye kumpenda Al Hassan na Al Hussein amenipenda na mwenye kuwachukia amenichukia."

3537715

captcha