Papa Francis ameeleza kusikitishwa na mashambulizi hayo dhidi ya
Waislamu wa Rohingya wa nchini Mynamar na kusema kuwa: Watu wote
wanapaswa kusaidia ili kufanikisha kukomeshwa mashambulizi na hatua za
ukandamizaji dhidi ya Waislamu wa Myanmar. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Waislamu wa kabila la Rohingya ni jamii ya wachache duniani inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi. Serikali ya Myanmar inakataa kuwapa haki za uraia Waislamu hao ambao idadi yao ni zaidi ya watu milioni moja na laki tatu.
Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Thailand, Malaysia na Indonesia kutokana na mashambulio ya Mabuddha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo.
3463768