IQNA

Harakati za Nujaba, Hizbullah nchini Iraq zaunga mkono IRGC

14:37 - April 11, 2019
Habari ID: 3471910
TEHRAN (IQNA)- Harakazi za mapambano ya Kiislamu Iraq ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi zimelaani vikali, hatua ya uhasama ya mtawala wa Marekani Donald Trump ya kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) nchini Iran katika orodha ya makundi ya kigaidi.

Msemaji wa vikosi vya Hizbullah nchini Iraq Sayyid Ja'afar al-Husseini sambamba na kulaani vikali, hatua ya uhasama ya Trump ya kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika orodha ya makundi ya kigaidi, amesisitiza kwamba jeshi hilo la Iran daima limesimama pamoja na mataifa ya eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) katika kufelisha njama chafu za Washington.

Sayyid Ja'afar al-Husseini ameongeza kwamba kufuatia hatua hiyo muqawama wa Iraq daima utasimama bega kwa bega na jeshi hilo la Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran kwa ajili ya kukabiliana na aina yoyote ya njama za mabeberu katika eneo hili. Kabla ya hapo pia Msemaji wa vikosi vya Hizbullah nchini Iraq alinukuliwa akisema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, waliokuwa waungaji mkono pekee kwa taifa la Iraq katika kukabiliana na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS).

Kwingineko,  Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Al-Nujaba nchini Iraq ametoa radiamali kali kufuatia hatua hiyo ya kiuhasama ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na amebainisha kwamba hatua hiyo ya Washington haitakuwa na taathira yoyote kwa makundi ya muqawama wa Kiislamu nchini Iraq na wala kwa jeshi hilo la Iran. Akibainisha kwamba uamuzi huo wa Trump ni sehemu ya hatua chafu za Marekani katika kuiwekea vikwazo vya upande mmoja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Hashim al-Musawi amesisitiza kwamba Iraq kamwe haitofuata vikwazo vya upande mmoja vya Washington dhidi ya Iran. Jumatatu ya jana Trump kupitia taarifa iliyosambazwa na White House aliliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC nchini Iran katika orodha ya makundi ya kigaidi hatua ambayo imeendelea kulaaniwa ndani na nje ya Marekani. Inafaa kuashiria kuwa, jeshi hilo la IRGC limekuwa na nafasi kubwa sana katika kuendesha mapambano makali dhidi ya makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati kama vile genge la Daesh (ISIS) Jab'hatu Nusra, Jaishu al-Sham na mengineyo.

Siku ya Jumatatu, utawala wa Marekani ulitangaza kuliweka Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika orodha yake ya makundi ya kigaidi. Uamuzi huo umechukuliwa ikiwa ni katika kuendeleza uhasama dhidi ya Iran na ni mashinikizo dhidi ya vikosi ambavyo, kwa kupambana na makundi ya kigaidi, vimefelisha  stratijia ya Washington katika eneo.

Kufuatia uhasama huo wa Marekani, Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetangaza kuwa, wanajeshi wote wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi (CENTCOM) na vikosi vyote vinavyofungamana nao ni kundi la kigaidi.

3468274

captcha