IQNA

Kufuatia dikrii ya Kiongozi Muadhamu
7:58 - January 04, 2020
News ID: 3472331
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Iran amemteua Brigedia Jenerali Esmail Qaani kuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Katika dikrii ya siku ya Ijumaa, Amiri Jeshi Mkuu amesema kufuatia kuuaawa shahidi Jenerali Soleimani mwenye hadhi ya juu, amemtaua Brigedia Jenerali Esmail Qaani kuwa kamanda wa kikosi cha Quds cha IRGC

Katika dikrii yake hiyo Kiongozi Muadhamu amemtaja Brigedia Jenerali Esmail Qaani kuwa kati ya makamanda waliopata mafanikio katika IRGC wakati wa zama za kujihami kutakatifu, na kwa muda mrefu amekuwa akifanya kazi kwa pamoja na Shahidi Soleimani. Ayatullah Khamenei amesema harakati za Kikosi cha Quds cha IRGC ziendelee kama ilivyokuwa wakati wa usimamizi wa Shahidi Soleimani. Aidha ametoa wito kwa maafisa wote wa Kikosi cha Quds cha IRGC  kushirikiana na Brigedia Jenerali Qaani.

Luteni Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes waliuawa shahidi mapema jana Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuwa, mtawala wa nchi hiyo, Donald Trump, ndiye aliyetoa amri ya kuuawa Jenerali Qassem Soleimani. Kitendo hicho cha kigaidi cha Marekani kinaendelea kulaaniwa kimataifa.

3868602  

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: