IQNA

Brigedia Jenerali Qaani

Shahidi Qassem Soleimani ni shujaa wa taifa la Iran, Umma wa Kiislamu

18:45 - January 01, 2021
Habari ID: 3473513
TEHRAN (IQNA) - Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) nchini Iran amesema kuwa Shahidi Qassem Soleimani ni shujaa wa taifa la Iran, Umma wa Kiislamu na vilevile shujaa wa kuyashinda madola ya kibeberu na kuongeza kuwa, njia ya Kikosi cha Quds na wanamuqawama haiwezi kubadilishwa kwa ushetani wa Marekani.

Brigedia Jenerali Esmail Qaani ameyasema hayo leo Ijumaa hapa mjini Tehran katika shughuli ya mwaka wa kwanza wa kukumbuka mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Abu Mahdi al Muhandis na wenzao kadhaa. Amesisitiza kuwa adui alikuwa akimsaka kwa udi na uvumba Luteni Jenerani Soleimani kwa kipindi cha miaka 30 na kuongeza kuwa: Mtu huyu punguani (Donald Trump) ndiye muovu na mtenda jinai mkubwa zaidi duniani ambaye hajali mpaka wa aina yoyote; na kutokana na ushawishi wa ushetani wa utawala haramu wa Israel na utawala wa Saudia, alitenda jinai isiyo na mfano duniani ambayo haijafanywa kwa shakhsia yeyote wa kisiasa na kijeshi katika zama hizi.

Brigedia Jenerali Qaani amewaambia Wamarekani kuwa: Wale waliotenda jinai hiyo wanapaswa kuelewa kwamba, wamefanya jambo ambalo popote pale watakapokuwa katika dunia hii atatokeza mtu atakayetoa jazaa na malipo stahiki kwa waovu hao. 

Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Kwa jinai hiyo mliyofanya mmetengeza kazi nyingine kwa watu huru duniani, na eleweni kwamba, hata ndani ya majumba yenu nyinyi wenyewe yumkini akajitokeza mtu atakayetoa jibu kwa jinai na uhalifu huo. 

Brigedi Jenerali Qaani ameashiria wahka na woga wa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mipaka ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kusema: Syria inaendelea kusimama kidete na hii leo karibu ardhi yote ya nchi hiyo imekombolewa; Iraq ya jihadi inaendelea kusimama imara na Yemen iliyodhulumiwa bado inapiga hatua madhubuti; hii ndiyo njia ya Shahidi Soleimani ambayo itaendelea kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu. 

Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Abu Mahdi al Muhandis ambaye alikuwa naibu mkuu wa harakati ya wananchi wa Iraq ya al Hashul Shaabi na wenzao 8 waliuawa shahidi tarehe 3 Januari mwaka 2020 kwa shambulizi la anga la wanajeshi magaidi wa Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq. Jenerali Soleimani alikuwa Iraq kwa mwaliko rasmi wa aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo. 

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) alielekea Iraq Januari 3 mwaka 2020 kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa Iraq.

Punde baada ya kuwasili Iraq aliuawa shahidi katika hujuma ya ndege za kivita za jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad. Aidha katika hujuma hiyo ya kigaidi Abu Mahdi Al Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati ya Kujitolea ya Wananchi wa Iraq, naye pia aliuawa shahidi akiwa ameandamana na Qassem Soleimani. Watu wengine wanane waliokuwa katika msafara huo nao pia waliuawa shahidi.

Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa na nafasi kubwa katika mapambano na maadui pamoja na magaidi na pia katika kuangamiza kundi la kigaidi la Daesh au ISIS. Pia alikuwa nguzo muhimu katika harakati za kupigania ukombozi wa Palestina. Halikadhalika alikuwa na nafasi muhimu katika kusambaratisha njama ya Marekani na Wazayuni ya kuligawa eneo vipande vipande.

3944758

Kishikizo: QAANI Soleimani irgc quds
captcha