IQNA

Sheria mpya ya uraia; changamoto kubwa kwa demokrasia India

20:00 - March 02, 2020
Habari ID: 3472524
TEHRAN (IQNA) – India inatambuliwa kama nchi ya kidemokrasia yenye muujiza wa kisasa kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu wa kaumu, kabila na dini mbali mbali wamekuwa wakiishi pamoja

Weledi wa mambo ya kisiasa wanaitaja India kuwa kitovu cha demokrasia kubwa zaidi duniani. Pamoja na hayo, sheria mpya ya uraia India, katika nchi yenye mamia ya makabila au kaumu  ni changamoto kubwa kwa nchi hiyo.

Sheria hiyo mpya ya uraia inaruhusu kupatiwa uraia wahajiri wa jamii za Wahindu, Mabudha na hata Wakristo wanaotokea katika nchi jirani za Pakistan, Bangladesh na Afghanistan, huku ikizuia kupewa uraia Waislamu wanaotoka katika nchi hizo.

Katiba yatumiwa kupinga sheria ya kibaguzi

Watu wa India wamepinga sheria hiyo mpya ya uraia na kusema inakinzana na katiba ya nchi hiyo. Wanaoshiriki katika maandamano wameonyesha nembo za utaifa zinazotambuliwa na katiba kama vile bendera na wimbo wa taifa. Maandamano hayo yanaonyesha kuwa sheria hiyo mpya ya uraia India ambayo ni maarufu kama  (NRC) ni tishio la kimsingi kwa taifa la India.

Fikra anuai za wapinzani

Maandamano ya kupinga sheria hiyo yalianza katika majimbo ya kaskazini mashariki hasa jimbo la Assam. Kwa waandamanaji wa kaskazini mashariki mwa India na Waislamu nchini humo, mapambano dhidi ya sheria hiyo mpya ya uraia ni sawa na kupigania utambulisho na uwepo wao lakini kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, wasomi na wanaharakati wa kijamii India, upinzani wao kwa sheria hiyo mpya ya uraia ni jambo la kiidiolojia.

Ukandamizaji wa haki za waliowachache

Sheria hiyo mpya ya uraia India inaidhinisha kupatiwa uraia wahajiri wa jamii za Wahindu, Mabudha na hata Wakristo wanaotokea katika nchi jirani za huku ikizuia kupewa uraia Waislamu wanaotoka katika nchi hizo inalenga kuoneysha kuwa Waislamu ni raia wa daraka la pili. Hii ndio sababu iliyopelekea Waislamu wajitokeze kwa wingi kupinga sheria hiyo.

Vita vya taasubi

Utumiaji mabavu waandamanaji ulifika kileleni wiki iliyopita wakati Kapil Mishra mmoja wa wanasiasa wanaofungamana na chama tawala cha BJP nchini India alipotangaza kuwa, iwapo polisi hawatazima maandamano ya kupinga sheria ya uraia, basi yeye na wafuasi watayazuia.  Masaa machache baada ya tangazo hilo la Mishra, wafuasi wake waliwashambulia waandamanaji. Katika kipindi cha siku kadhaa zilizopita wafuasi hao wa BJP wameteketeza moyo misikiti, nyumba na maduka ya Waislamu na hadi sasa watu wasiopungua 40 wamepoteza maisha wengi wakiwa ni Waislamu.

3882645

Sheria mpya ya uraia; changamoto kubwa kwa demokrasia India

Sheria mpya ya uraia; changamoto kubwa kwa demokrasia India

Sheria mpya ya uraia; changamoto kubwa kwa demokrasia India

captcha