Wataalamu wanasema kupata nguvu vyama vya upinzani kutaleta kiwango fulani cha faraja kwa Waislamu nchini India, ambao wamekabiliwa na miaka kadhaa ya ubaguzi uliokithiri chini ya serikali ya Modi yenye misimamo mikali ya utaifa wa Kihindu wa kibaniani ujulikanao kama Hinduvata
Akizungumza na Middle East Monitor, P. K. Niaz, mwandishi wa habari mwandamizi aliyeko Qatar, amesema wakati Narendra Modi na washirika wake wa utaifa wa Kihindu wamesalia na mamlaka katika uchaguzi mkuu wa India, mafanikio makubwa ya vyama vya upinzani yatatoa faraja kwa kiwango fulani kwa Waislamu walio wachache nchini humo ambao imekabiliwa na miongo kadhaa ya ubaguzi na ukandamizaji wa Wahindu wenye misimamo mikali.
Matokeo rasmi ya yaliyochapishwa wiki hii Tume ya Uchaguzi ya India yalithibitisha kuwa muungano wa Modi wa National Democratic Alliance (NDA), ambao unajumuisha chama chake cha mrengo wa kulia cha Hindutva, Bharatiya Janata Party (BJP), ulishinda viti 294, ikiwa ni zaidi ya viti 272 vinavyohitajika ili kupata uongozi wa bunge, lakini ni chini ya ilivyotarajiwa. Kwa mara ya kwanza tangu BJP ilipoingia madarakani mwaka wa 2014, haikupata wingi wa kura peke yake, ikishinda viti 240, chini ya rekodi 303 iliyoshinda katika uchaguzi wa 2019. Muungano wa upinzani unaoongozwa na Chama cha Congress uonojulikana kama, INDIA, ambao unaungwa mkono kikamilifu na Waislamu, ulipata viti 223.
Hii inaonyesha kwamba Modi lazima ategemee uungwaji mkono wa washirika wake wa muungano, kikiwemo Chama cha Telugu Desam (TDP) kusini mwa jimbo la Andhra Pradesh chenye viti 16, na Janata Dal (United), ambacho kilishinda viti 12 katika jimbo la Bihar mashariki, na vile vile vyama vingine vidogo vidogo.
Hili ni pigo la kushangaza kwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73, ambaye alitarajia ushindi wa kishindo.
Wakati wa kampeni za uchaguzi, Modi alitabiri kuwa chama chake kingeshinda viti 370 na kuvuka alama 400 kwa kuungwa mkono na washirika wake.
Wakati wa kampeni za uchaguzi, Modi alitumia maneno ya chuki dhidi ya Waislamu katika hotuba zake kote India. Wataalamu wa siasa za India wanasema hakuna waziri mkuu katika historia ya India aliyeshusha hadhi ya ofisi yake kama Modi.
Matokeo ya hayo ya uchaguzi yanaonyesha kuwa magenge Hindutva ya Modi, ambayo huwashambulia Waislamu, hayawezi tena kuwa na mkono huru katika kutekeleza ajenda yao dhidi ya Uislamu.
Kwa kuwa chama chake hakina wingi wa kura, ni lazima Modi apambane na upinzani mkali bungeni, na atalazimika kupata uungaji mkono wa washirika wake kabla ya kufanya maamuzi muhimu. Hili linaweza kumlazimisha kutumia mbinu tahadhari na mashauriano zaidi katika kufanya maamuzi yake. Pia sasa atalazimika kupunguza kasi ya ajenda yake dhidi ya Uislamu iwapo anataka kutawala bila matatizo.
3488645