IQNA

Waislamu India

Pakistan yataka UN ilinde maeneo ya Kiislamu India baada ya kubomolewa kwa Misikiti

21:17 - February 10, 2024
Habari ID: 3478329
IQNA - Pakistan imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuingilia kati na kulinda misikiti na maeneo ya turathi ya Kiislamu nchini India, kufuatia kuharibiwa kwa msikiti wa kihistoria wa Akhunji mjini New Delhi wiki iliyopita.

Msikiti huo wa karne nyingi ulibomolewa na Mamlaka ya Maendeleo ya Delhi (DDA) mnamo Januari 30, bila taarifa yoyote ya awali kwa jumuiya ya Waislamu wa eneo hilo, wasimamizi wa msikiti, au wanafunzi wa Madressah waliosoma hapo.

DDA, ambayo iko chini ya serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi, imedai msikiti huo umejengwa kwenye hifadhi ya msitu, madai ambayo yanapingwa na kamati ya msikiti.

Seminari ya Kiislamu na makaburi yaliyounganishwa na msikiti huo pia yaliharibiwa, huku polisi na vikosi vya kijeshi vikizingira eneo hilo.

Katika barua kwa Muungano wa Ustaarabu  wa Umoja wa Mataifa (UNAOC), Balozi wa Pakistan Munir Akram alilaani ubomoaji huo na kusema kuwa ni kitendo cha  uhalifu cha itikadi kali ya Kihindu na ni sehemu ya kampeni ya kutisha inayolenga maeneo ya Kiislamu nchini India, The Nation liliripoti Jumamosi.

Alisema misikiti mingine kadhaa imebomolewa au iko hatarini kubomolewa na mamlaka ya India au makundi ya Wahindu wenye msimamo mkali.

Alitahadharisha kuwa uungaji mkono wa serikali kwa matukio hayo ni tishio kubwa kwa ustawi wa Waislamu wa India katika nyanja zote za maisha. Pia aliashiria ushawishi wa itikadi ya Kihindu ya  'Hindutva' na kuongezeka kwa chuk dhidi ya Uislamu nchini India na kusema kuna haja ya jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kuzuia maafa.

Kiongozi wa kiroho Imam wa msikiti wa Akhonji, Imam Zakir Hussain, alielezea masikitiko yake kutokana na kupoteza msikiti huo, ambao alisema sio tu kuwa sehemu ya ibada bali pia Madrassah na makaburi ya watu wanaoheshimika.

Msikiti huo uliaminika kuwa na umri sawa na eneo la Qutub Minar, jengo la karne ya 13 Miladia ambalo liko katika orodha turathi ya dunia ya UNESCO katika eneo la Mehrauli huko Delhi.

3487137

Kishikizo: india bjp waislamu msikiti
captcha