IQNA

Shughuli za Qur'ani

Kuba la Musa; Kituo cha kwanza cha Mafunzo ya Qur'ani huko Palestina

21:12 - November 19, 2024
Habari ID: 3479775
IQNA – Kuba la Musa katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji mtakatifu wa al-Quds linachukuliwa kuwa kituo cha kwanza cha kufundisha Qur'ani huko Palestina.

Ni kuba la zama za Ayyubi lililoko katikati ya Jukwaa la Musa katika ua la magharibi wa Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem).
Kuba hiyo ilijengwa na Sultan Salih Najmeddin Ayyub, mfalme wa mwisho wa nasaba ya Ayyubi, mnamo 1249 Miladia.
Jumba la Musa ni jengo la mwisho kujengwa msikitini wakati wa enzi ya Ayyubi.
Sultan Salih Ayyub anajulikana kama mkombozi wa pili wa al-Quds, kwa vile aliuteka tena mji huo kutoka kwa Wanajeshi wa Msalaba baada ya baba yake kuukabidhi kwa wapiganaji hao mwaka 1229 chini ya Mkataba wa Yafa.
Kuna maelezo tofauti ya kwa nini jengo hilo linaitwa Kuba ya Musa. Wengine wanasema lilipewa jina la mmoja wa masheikh walioongoza swala katika jengo hilo. Wengine wanaamini inamhusu Amir Musa bin Hassan al-Hadbani, ambaye alisimamia ujenzi wa ua wa magharibi wa msikiti huo mnamo 1337.
Kwa mujibu wa maelezo mengine, Sultan Salih Ayyub aliita jina hilo kwa ajili ya kumuenzi Nabii Musa (AS).
Jengo hilo lina chumba cha mita 7 kwa 7 na kuba hiyo iko kwenye safu ya hexagonal.
Ina madirisha 6 na Mihrab katika ukuta wa kusini. Milango iko upande wa kaskazini.
Katika miaka ya mwisho ya kipindi cha Mamluk, Jaji Mujiruddin Hanbali alitumia jengo hilo kama mahakama. Wakati wa Ufalme wa Ottoman, ilitumika kwa sherehe za Sama.
Mnamo mwaka wa 2024, Kuba ya Musa ilirejea katika kazi yake ya zamani, ikitumika  kama kituo cha kufundisha Qur’ani.
Hivi sasa inaandaa darsa nyingi za usomaji na kuhifadhi Qur’ani.

3490742

Habari zinazohusiana
Kishikizo: al aqsa qurani tukufu
captcha