IQNA

12:01 - May 21, 2020
News ID: 3472789
TEHRAN (IQNA) – Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya muqawama (mapambano) ya Lebanon amesema utawala wa Kizayuni wa Israel umeingiwa na wasiwasi mkubwa kutokana na ushindi wa mhimili wa muqawama.

Ameongeza kuwa harakati hiyo itaendelea kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina na katu haitotelekeza Quds kwa gharama yoyote ile. 

Sayyid Hasan Nasrallah alisema hayo jana Jumatano katika hotuba aliyoitoa kwa mnasaba wa kukaribia Siku ya Kimataifa ya Quds itakayoadhimishwa Ijumaa ya kesho na kuongeza kuwa, "wanaopania kuufanya wa kawaida uhusiano na utawala wa Kizayuni sio wawakilishi halisi wa umma wa Kiislamu."

Amebanisha kuwa, "mwaka huu tunamkosa mmoja wa makamanda wakuu walioipigania Quds, Haji Qassem Soleimani. Tulimuahidi Shahidi Soleimani kwamba tutaikomboa Palestina na tutasawalia Quds Tukufu."

Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu itakuwa ni Ijumaa ya tarehe 28 Ramadhani, 1441 Hijria inayosaidiana na Mei 22, 2020 Miladia.

Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu hayati Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) ndiye aliyeipa siku hiyo ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi Ramadhani jina la Siku ya Kimataifa ya Quds kwa shabaha ya kuakisi dhulma ya kihistoria inayofanywa na Israel, kwa himaya ya madola ya Magharibi yanayodai kutetea haki za binadamu, dhidi ya watu wanaoendelewa kudhulumiwa na kukandamizwa wa Palestina na ardhi yao takatifu. Tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979, Siku ya Kimataifa ya Quds imekuwa ikiadhimishwa kupitia maandamano na makongamano  kote duniani.

Kwa wale wanaotaka kushiriki katika Siku ya Kimataifa ya Quds  wanaweza kushiriki katika mjumuiko wa intaneti Ijumaa Mei 22 kuanzia saa 10-12 kwa saa za Uingereza kwa njia ya YouTube na Facebook kupitia anuani ya #AlQudsDay2020.

3900465

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: