IQNA

Taarifa ya Harakati ya Mshikamano wa Kenya na Palestina
19:17 - May 22, 2020
News ID: 3472792
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Mshikamano wa Kenya na Palestina (KPSM) imetoa taarifa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds na kusisitiza kuwa Wapalestina wanakabiliana na virusi viwili hivi sasa.

Katika taarifa, mwenyekiti wa  Harakati ya Mshikamano wa Kenya na Palestina Zahid Rajan amesema: “Leo Wapalestina wanakabiliana na virusi viwili, kwanza ni kirusi cha utawala wa kibaguzi wa Israel na pili ni kirusi cha COVID-19 na wanapaswa kuagamiza virusi vyote  hivyo viwili.” Rajani aidha amesisitiza kuhusu haki ya Wapalestina kurejea katika ardhi zao za jadi na kuondolewa mzingiro wa Ukanda wa Ghaza.

Mwenyekiti wa Harakati ya Mshikamano wa Kenya na Palestina aidha amesema wanapinga vikali ‘Muamala wa Karne’ na kusema  muamala pekee ambao unatakiwa ni ule wa ukombozi wa Palestina.

Halikadhalika ametoa wito kwa wanaharakati wote Palestina kuwa na lengo la pamoja na  ukombozi na hivyo wanapaswa kupinga njama zote za kuibua mgawanyiko baina yao.

Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu imeadhimishwa leo  Ijumaa ya tarehe 28 Ramadhani, 1441 Hijria inayosaidiana na Mei 22, 2020 Miladia.

Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu hayati Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) ndiye aliyeipa siku hiyo ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi Ramadhani jina la Siku ya Kimataifa ya Quds kwa shabaha ya kuakisi dhulma ya kihistoria inayofanywa na Israel, kwa himaya ya madola ya Magharibi yanayodai kutetea haki za binadamu, dhidi ya watu wanaoendelewa kudhulumiwa na kukandamizwa wa Palestina na ardhi yao takatifu.

3471493

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: