IQNA

11:45 - May 21, 2020
News ID: 3472788
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amelaani vikali jaribio la baadhi za tawala za Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kiongozi wa Ansarullah, Sayyid Abdul-Malik Badreddin al Houthi ameyasema hayo Jumatano katika hotuba aliyotoa kwa kwa njia ya video kwa mnasaba wa kukaribia Siku ya Kimataifa ya Quds. Amesema kuwa na uhusiano na utawala huo pandikizi ni kupuuza kadhia muhimu ya Umma wa Kiislamu yaani kadhia ya Palestina. Ameeleza bayana kuwa, "sababu ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni kutokana na nafasi yake muhimu yake katika kupambana na adui Mzayuni na Marekani." Aidha ametoa wito wa kususiwa bidhaa za Marekani na utawala bandia wa Israel. Kiongozi wa Ansarullah amesema Siku ya Kimataifa ya Quds ni ubunifu wa Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu Amrehemu), muasisi wa  Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa lengo la kuwakumbusha Waislamu majukumu yao kuhusu mji wa Quds (Jerusalem), ambao unakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah amesema taifa la Yemen liko imara katika kuwaunga mkono Wapalestina.

Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu itakuwa ni Ijumaa ya tarehe 28 Ramadhani, 1441 Hijria inayosaidiana na Mei 22, 2020 Miladia.

Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu hayati Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) ndiye aliyeipa siku hiyo ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi Ramadhani jina la Siku ya Kimataifa ya Quds kwa shabaha ya kuakisi dhulma ya kihistoria inayofanywa na Israel, kwa himaya ya madola ya Magharibi yanayodai kutetea haki za binadamu, dhidi ya watu wanaoendelewa kudhulumiwa na kukandamizwa wa Palestina na ardhi yao takatifu. Tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979, Siku ya Kimataifa ya Quds imekuwa ikiadhimishwa kupitia maandamano na makongamano  kote duniani.

Kwa wale wanaotaka kushiriki katika Siku ya Kimataifa ya Quds  wanaweza kushiriki katika mjumuiko wa intaneti Ijumaa Mei 22 kuanzia saa 10-12 kwa saa za Uingereza kwa njia ya YouTube na Facebook kupitia anuani ya #AlQudsDay2020.

3900460

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: