IQNA

Qiraa ya Qur’ani Tukufu ya qarii mashuhuri wa Algeria

16:17 - May 06, 2020
Habari ID: 3472740
TEHRAN (IQNA) – Qarii mashuhuri wa Qur’ani Tukufu kutoka Algeria, Sheikh Muhammad bin Sudaira hivi karibuni alisoma aya za Qur’ani Tukufu kuhusu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Qarii bin Sudaira amelitumia Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) faili ya qiraa yake ya aya za 183 na 185 za Qur’ani Tukufu.

Qarii huyu wa Algeria ameshiriki katika mashindano kadhaa ya Qur’ani ya kimataifa ambapo alishika nafasi ya kwanza katika Mashindani ya Kimataifa ya Qur’ani ya Tunisia na nafasi ya pili katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Qatar.

Siku chache zilizopita pia alisoma aya za Surah Maryam katika Televisheni ya Al Kauthar ya Iran akiwa mshiriki wa mashindano ya Qur’ani ya Mwezi wa Ramadhani katika televisheni hiyo yanayojulikana kama إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا , "Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu".  (Qur’ani Tukufu 78:31).

3896659

captcha