IQNA

Jinai za Israel

Al-Azhar yalaani uhalifu wa Utawala wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi, yataka Israel isusiwe

22:35 - September 01, 2024
Habari ID: 3479363
IQNA - Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimelaani vikali kushadidi jinai za utawala wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, Al-Azhar ilisisitiza haja ya kususia bidhaa za utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mshikamano na taifa la Palestina.

Ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kupigia debe kampeni ya kugomea bidhaa za Israel kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa wa Palestina, Msikiti wa Al-Aqsa na mji mtakatifu wa al-Quds, ilisema taarifa ya Al Azhar.

Taarifa hiyo pia ilionya juu ya njama za utawala wa Israel za kutaka kuyahudisha Ukingo wa Magharibi, iliripoti Al Jazeera.

Tangu kuanza kwa uvamizi wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7, 2023, Ukingo wa Magharibi pia umeshuhudia kuongezeka kwa ghasia kutoka kwa vikosi vya Israeli na walowezi ambao waligharimu maisha ya mamia ya Wapalestina.

Mapema siku ya Jumatano, jeshi la utawala dhalimu wa Israel lilifanya operesheni yake kubwa zaidi - iliyoitwa "Kambi za Majira ya joto" - katika Ukingo wa Magharibi katika zaidi ya miaka 20, kwa kupeleka mamia ya askari na mashambulizi ya anga kwenye Jenin, Tulkarem, na Tubas, ambayo ni vituo kuu vya wanamapambano wa Palestina  dhidi ya utawala huo ghasibu.

3489726/

Habari zinazohusiana
Kishikizo: israel al azhar
captcha