IQNA

Mashindano ya Qur’ani kwa Wanafunzi wa Kigeni wa Al-Azhar yapongezwa

14:22 - November 20, 2025
Habari ID: 3481544
IQNA – Jumuiya ya Kimataifa ya Wahitimu wa Al-Azhar imeandaa mashindano ya usomaji wa Qur’an ya “Sauti Njema” nchini Misri, tukio lililopokelewa kwa furaha na wanafunzi wa Al-Azhar kutoka mataifa mbalimbali.

Mashindano hayo yaliwahusisha wanafunzi wa Al-Azhar kutoka Misri na nje ya Misri, na yalifanyika katika muktadha wa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jumuiya ya Kimataifa ya Wahitimu wa Al-Azhar na Taasisi ya Hisani ya Abu Al-Ainin Shuaisha, kwa lengo la kuunga mkono programu za kitamaduni na kuwatambua vijana wenye vipaji chipukizi katika Qur’ani Tukufu, kwa mujibu wa taarifa ya El-Balad.

Saad Al-Mutani, mkurugenzi wa idara ya vyombo vya habari ya jumuiya hiyo na msimamizi wa mashindano, alisema kuwa taasisi yao inaendelea kuunga mkono vipaji vya Qur’ani kati ya wanafunzi wa Al-Azhar kupitia juhudi kama tukio la Qur’ani la “Sauti Njema”.

Aliongeza kuwa ushirikiano na Taasisi ya Shuaisha ni dalili ya dhamira ya dhati ya kushirikiana katika kuwasaidia wanafunzi wa Al-Azhar wa kigeni na wale wa Misri, sambamba na kuwapa fursa ya kuonesha uwezo wao kwa namna inayoendana na hadhi tukufu ya Al-Azhar na dhamira yake ya kielimu.

Mashindano hayo yalifanyika katika Kituo cha Sheikh Zayed cha Kufundisha Kiarabu kwa Wasiokuwa Waarabu nchini Misri, na yaliendelea kwa muda wa siku mbili.

Yalipokelewa vyema na washiriki kutoka mataifa mbalimbali, na yakachukuliwa kuwa ni hatua muhimu katika kutambua na kukuza vipaji vipya katika usomaji wa Qur’ani, pamoja na kuimarisha hadhi ya ndani na ya kimataifa ya Jumuiya ya Kimataifa ya Wahitimu wa Al-Azhar.

Inafaa kufahamu kuwa Taasisi ya Abu Al-Ainin Shuaisha ni taasisi huru ya kijamii na kihadhi iliyoanzishwa mwaka 2001 na Kikundi cha Cleopatra nchini Misri.

Hadi sasa, imefadhili na kutekeleza miradi mbalimbali ya afya, elimu na kijamii kwa lengo la kuimarisha ustawi wa jamii ya Misri.

4317905

 

Habari zinazohusiana
captcha