IQNA

Hizbullah yakosoa gazeti la Saudia lililomvunjia heshima Ayatullah Sistani

12:19 - July 05, 2020
Habari ID: 3472931
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imelaani vikali hatua ya gazeti moja linalomilikiwa na Saudia kuchora katuni inayomvunjia heshima kiongozi wa juu wa kidini wa nchini Iraq Ayatullah Sayyed Ali Al-Sistani.

Katika taarifa Jumamosi, Hizbullah imeashiria hadi ya Ayatullah Sistani miongoni mwa Waislamu na kumtaja kuwa mhimili wa umoja wa uthabiti nchini Iraq.

Hizbullah imesema kitendo kama hicho cha gazeti la Saudia hakiwezi kuathiri nafasi ya kihistoria ya mwanazuoni huyo wa Kiislamu.

Malalamiko makubwa na upinzani mkali wa viongozi na mirengo tofauti ya kisiasa ya Iraq, sambamba na hatua nyingi zilizochukuliwa na wananchi na makundi ya muqawama wa Kiislamu katika mitandao ya kijamii dhidi ya hatua ya gazeti la Kisaudi la Ash-Sharqul-Awsat ya kuchora katuni ya kumvunjia heshima kiongozi wa juu wa kidini wa nchini Iraq, hatimaye zimepelekea gazeti hilo lilazimike kuondoa katuni hiyo.

Tovuti ya kanali ya televisheni ya Sumaria News ya nchini Iraq imeripoti kuwa, gazeti la Ash-Sharqul-Awsat lilitoa taarifa hapo jana Jumamosi likidai kwamba, baadhi ya vituo vya habari vya Iraq viliamua kwa makusudi kuipa madhumuni na mtazamo ambao sio uliokusudiwa katuni hiyo iliyochapishwa na gazeti hilo siku ya Ijumaa.

Katika tarifa hiyo ya kutetea hatua yake ya kuondoa katuni hiyo inayomvunjia heshima Ayatullah Sistani, gazeti hilo la Kisaudi limedai kuwa, linaheshimu na kuchunga kanuni za taaluma ya yake ya habari kuhusiana na nchi, shakhsia na viongozi wa juu wa kidini; na kwamba katuni hiyo haikuwa inamuashiria kwa namna yoyote ile Sayyid Ali Sistani, Marjaa Taqlidi wa nchini Iraq kwa sababu alimu huyo ni shakhsia wa kuenziwa na kuheshimiwa.

Uamuzi huo wa Ash-Sharqul-Awsat umechukuliwa wakati siku ya Ijumaa gazeti hilo la utawala wa Aal Saud lilichapisha picha ya katuni iliyomtusi na kumvunjia heshima Ayatullah Sistani, kiongozi wa juu wa kidini mwenye hadhi ya juu nchini Iraq hatua ambayo ilikabiliwa na upinzani na malalamiko ya mirengo na makundi mbali mbali ya kisiasa na kijamii ya nchi hiyo ya kulaani hatua hiyo ya kiafiriti.

 3908648

Kishikizo: Ayatullah Sistani ، iraq ، Saudia ، Hizbullah
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha