IQNA

Qarii Mtanzania ashinda Mashindano ya Qur’ani ya Sharjah

23:07 - August 01, 2020
Habari ID: 3473023
TEHRAN (IQNA) – Qarii kutoka Tanzania ameibuka mshindi katika mashindano ya kusoma Qur’ani (qiraa) ya Chuo Kikuu cha Al Qasimia cha Sharjah katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Zaidi ya wanachuo 100 kutoka vitivo mbali mbali vya chuo hicho walishiriki katika mashindano hayo  ambapo Hamza Abubakr Swaleh wa Tanzania, ambaye anasoma katika Kitivo cha Qur’ani, aliibuka mshindi.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Abdullah Bassam wa Lebanon huku Watun Buniako wa Kosovo. Mashindano hayo yaliandaliwa na Kitivo cha Qur’ani cha Chuo Kikuu cha Al Qasimia.

Mashindano hayo yanalenga kutambua vipaji vya Qur’ani miongoni mwa wanachuo sambamba na kuwahimiza kuhifadhi na kusoma Qur’ani. Mashindano hayo yalifanyika kwa njia ya video kutokana na vizingiti vilivyowekwa baada ya kuibuka ugonjwa wa corona.

3913793

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha