IQNA

Jinai za Israel

Quds yageuzwa na Israel kuwa eneo la kijeshi kabla ya uchochezi wa 'Maandamano ya Bendera'

16:15 - June 04, 2024
Habari ID: 3478929
IQNA – Utawala ghasibu wa Israel umegeuza mji unaokaliwa kwa mabavu wa al-Quds  (Jerusalem)  kuwa eneo la kijeshi kwa kisingizio cha kufanikisha mjumuiko wa kichochezi unajulikana kama "maandamano ya bendera". Mjumuiko huu umepengwa jumuiya za kikoloni siku ya Jumatano.

Israel umetuma zaidi ya polisi 3,000 kwenda kuikalia al-Quds, na kuweka vizuizi vya kijeshi kwenye barabara kuu, na kutangaza kufunga njia katika mkesha wa kile kinachoitwa "maandamano ya bendera," ambayo yatafanyika katika vitongoji vya Old al-Quds na kuishia katika al-Buraq.

Mawaziri na wajumbe la utawala haramu wa Israel, Knesset,  wanatarajiwa kushiriki katika maandamano hayo ya uchochezi.

Mashirika yanayodaiwa kuwa ya "Hekalu" na makundi ya kikoloni yametoa wito wa kuhujumiwa Msikiti wa Al-Aqsa Jumatano asubuhi.

Kamisheni ya Kikristo ya Kiislamu ya Kuunga mkono mji wa Quds na Matukufu yake imetahadharisha juu ya hatari ya hujuma yaIsrael dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa katika mkesha wa kuadhimisha kukaliwa kwa mabavu mji wa al-Quds.

Kamisheni hiyo imesema kwamba inachunguza kwa uzito wa hali ya juu juu ya kuongezeka kwa msikiti wa Al-Aqswa na jaribio la kuweka ukweli mpya ambao unadhoofisha hali ya kidini na kisheria iliyopo, na kuongeza kuwa inazishikilia mamlaka za uvamizi kuwajibika kikamilifu kwa athari mbaya za ukiukaji huu.

Imetoa wito kwa Waislamu wa Palestina kuhamasishwa na kuelekea  hadi Msikiti wa Al-Aqsa ili kukabiliana na jaribio lolote la wakoloni la kuuvamia na kufanya ibada za Kiyahudi ndani ya msikiti huo.

3488617

captcha