IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akiwahutubu vijana Wafaransa
11:27 - October 29, 2020
News ID: 3473306
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kushangazwa kwake na undumakuwili wa Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwa kulikingia kifua jarida la Charlie Hebdo la nchini hiyo ya Ulaya kwa kuchapisha tena vibonzo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW, kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza.

Katika ujumbe wake kwa vijana wa Ufaransa, Ayatullah Ali Khamenei amelitaka tabaka hilo limhoji Rais wao kwa kumuuliza, kwa nini anamtusi Mtume wa Mungu kwa jina la uhuru wa maoni? Na je, uhuru wa kujieleza una maana ya matusi, haswa kuwatukana watu watukufu?

Kadhalika Ayatullah Khamenei amewataka vijana wa Ufaransa wamsaili Rais wao, je, kwa nini ni jinai kutilia shaka Holocaust (mauaji yanayodaiwa kufanywa na Manazi) dhidi ya Wayahudi?

Kwa nini anayeandika juu ya kutiliwa shaka mauaji hayo (ya Holocaust) anafungwa jela, lakini kumtusi Mtume Mtukufu SAW kunaruhusiwa?

Hatua ya Rais Emmanuel Macron ya kutoa matamshi ya jeuri dhidi ya Uislamu na kutangaza kuwa, Ufaransa itaendelea kusambaza katuni na vibonzo vinavyomdhalilisha Mtume Muhammad (SAW), imeughadhabisha mno Umma wa Kiislamu.

Maandamano ya kulaani kitendo hicho yameshuhudiwa katika nchi kadhaa za Kiislamu na Kiarabu kama vile Iran, Iraq na Bangladesh, huku mwito wa kusisiwa bidhaa za Ufaransa katika nchi hizo ukishika kasi.

3931922

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: