IQNA

Wasomi na wanafikra wataka sheria za kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu

12:18 - November 05, 2020
Habari ID: 3473331
TEHRAN (IQNA)- Wasomi, wanafikra, wanaharakati na wanazuoni wa Kiislamu duniani wametoa wito wa kutungwa sheria zinazozuia kuvunjiwa heshima Mitume wa Mwenyezi Mungu, dini za mbinguni na wafuasi wake.

Kundi hilo la wanafikra na viongozi wa dini duniani limetangaza katika barua ya wazi kwa wasomi, wanafikra na watu wenye kuona mbali kote duniani hususan taifa la Ufaransa kwamba mwenendo wa aina yoyote unaosababisha kuvunjiwa heshima, kubaguliwa na chuki dhidi ya wanadamu, sawa kwa kisingizio cha kupigania uhuru na demokrasia au kwa kutumia mbinu za kimabavu na kidikteta, ni hatua inayopingana na uhuru wa mwanadamu.

Barua hiyo iliyoolewa jana imeashiria jinai na uhalifu uliofanywa na serikali ya Ufaransa katika miaka iliyopita ikiwa ni pamoja na mauaji ya zaidi ya Waalgeria milioni moja wakati wa mapambano ya ukombozi dhidi ya ukoloni wa Ufaransa katika muongo wa 1940, mauaji ya umati ya mamia ya raia wa Vietnam hapo tarehe 29 Novemba mwaka 1947 na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa na Ufaransa katika kipindi cha ukoloni wake katika nchi mbalimbali hususan barani Afrika na kuongeza kuwa: Ufaransa inapaswa kuwa ya mwisho na kushika mkia katika jitihada zinazofanywa na jamii ya wanadamu kwa ajili ya kutetea haki za binadamu, uhuru wa kusema na kujieleza na demokrasia.

Wasomi, wanafikra, wanaharakati na wanazuoni wa Kiislamu dunian pia wameashiria mwenendo wa jarida la Charlie Hebdo la Ufaransa wa kueneza chuki na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu, Uislamu na Mtume Muhammad (saw) mara kwa mara, na vilevile uungaji mkono Rais Emmanue Macron wa nchi hiyo kwa kitendo hicho kiovu na kusisitiza kuwa: Njama za kuzusha mifarakano baina ya wafuasi wa dini za mbinguni kupitia njia ya kuuhujumu Uislamu ni kanuni iliyokita mizizi katika fikra na aidiolojia ya Kimarekani na Kifaransa ambayo hii leo inadhihirika katika mbinu ya kutenganisha jamii ya Waislamu na wasio Waislamu, kupachika watu majina ya kutisha, ubaguzi wa kijamiii na katika ajira na mieneno ya kikatili ya polisi.

Barua hiyo imewataka wasomi na wanafikra wa Ufaransa, viongozi wa dini dunia hususan katika ulimwengu wa Kiislamu, Ukristo na Uyahudi kushirikiana kwa ajili ya kuzuia makabiliano baina ya wafuasi wa dini, mbari na kaumu tofauti.

Vilevile imeitaka Kamisheni Kuu ya Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa umoja huo na Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu kuzuia vitendo vya kuvunjiwa heshima Mitume wa Mwenyezi Mungu, dini za mbinguni na wafuasi wa dini hizo.

 

3473032

captcha