IQNA

Ufaransa yaonaya raia wake baada ya hujuma dhidi ya makaburi Jeddah, Saudia

10:47 - November 12, 2020
Habari ID: 3473352
Ufaransa yaonaya raia wake baada ya hujuma dhidi ya makaburi Jeddah, Saudia

Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema shambulio hilo lilitokea katika makaburi ya wasiokuwa Waislamu katika mji  Jeddah ulioko katika Bahari ya Sham.Hata hivyo, wizara hiyo haikutoa maelezo zaidi juu ya idadi ya majeruhi au uraia wako.

Kufuatia hujuma hiyo, Ubalozi wa Ufaransa katika Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, umewataka raia wake kuwa macho baada ya kutokea shambulio katika mji wa Jeddah. Taarifa kutoka ubalozi huo imesema, Ufaransa inawasiliana na mamlaka za UAE ili kuhakikisha raia wake wako salama.

Hujuma hiyo ya Jumatano inakuja huku  Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akiendelea kuwakasirisha Waislamu duaniani baada ya kuunga mkono wale wanaomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW katika nchi hiyo ya Ulaya.

Waislamu duniani wameandamana kote duniani kumlaani mtawala huyo wa Ufaransa huku wakitaka bidhaa za Ufaransa zisusiwe.

3473095

captcha