IQNA

Qiraa ya Qur'ani Tukufu ya Sheikh Noaina wa Misri

11:45 - November 28, 2020
Habari ID: 3473402
TEHRAN (IQNA)- Hivi karibuni, Televisheni ya Qur'ani ya Iran ilirusha hewani qiraa ya qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Ahmed Ahmed Noaina.

Katika klipu hii Sheikh Noaina anasema aya Qur'ani Tukufu kutoka katika Surah al-Insan, Surah ash-Shams na Surah al-Adiyat.

Sheikh Noaina  (Nuaina) alizaliwa mwaka 1954 katika mji wa Mutubas nchini Misri na alianza kujifunza Qur’ani Tukufu akiwa na umri wa miaka 4 na kuhifadhi Kitabu hicho Kitukufu akiwa na umri wa miaka minane.

Alijifunza mbinu ya qiraa ya Ustadh Mustafa Ismail huku akiendeleza masomo yake katika taalumu ya daktari wa watoto.

Noaina anatambuliwa kama mmoja kati ya wasomaji bora zaidi wa Qur’ani Misri na ulimwengu mzima katika zama hizi. Sheikh Daktari Nuaina ni qariii mtajika Misri na amepata umashuhuri kutokana na mbinu kumi tafauti anazotumia kusoma Qur'ani Tukufu.

Qarii huyu mashuhuri wa Misri amewahi kusoma katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Misri na nchi nyingi za Kiislamu. Mbali na kuwa msomaji wa Qur'ani pia amehifadhi kikamilifu kitabu hicho kitukufu. Taaluma nyingine ya Sheikh Nuaina ni daktari wa watoto.

3473243

captcha