IQNA

21:31 - December 06, 2020
Habari ID: 3473428
TEHRAN (IQNA) – Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ameahidi uwajibikaji wa serikali yake kuhusu ripoti ya hujuma dhidi msikiti mjini Christchurch.

Siku ya Jumapili, Ardern alikaa kwa muda wa masaa mawili na waathirika pamoja na familia za waliouawa katika hujuma hiyo kabla ya kuzinduliwa ripoti ya Tume ya Kifalme Kuhusu Mashambulizi Dhidi ya Misikiti Christchurch.

Katika hujuma dhidi ya misikitimiwili ya Christchurch Machi 15, mwaka jana, gaidi wa Kikristo aliwaua Waislamu 51 waliokuwa katika swala ya Ijumaa.

Mwezi Agosti Mahakama nchini New Zealand ilimhukumu kifungo cha maisha jela gaidi Brenton Tarrant baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua Waislamu hao 51.

Hakimu aliyetoa hukumu hiyo alikiri kuwa hiyo si adhabu tosha kwa jinai ya iliyotendwa na gaidi huyo mwenye itikadi kuwa wazungu ni wanadamu bora zaidi watu wengine wote.

Tarrant, raia wa Australia mwenye umri wa miaka 29, alikiri kutekeleza mauaji ya watu 51 na kujaribu kuwaua wengine 40 na pia amekiri kutekelezx akitendo cha kigaidi katika hujuma ya ufatuaji risasi kiholela dhidi ya misikiti miwili mjini Christchurch.

Gaidi Tarrant pia ni mfuasi sugu wa  Rais Donald Trump wa Marekani ambaye ni mashuhuri kwa chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Katika shambulizi la kigaidi la Machi 15 2019 katika misikiti ya Linwood na al-Noor mjini Christchurch, Waislamu 51 waliuawa shahidi na wengine karibu 50 kujeruhiwa.

Jaji Cameron Mander wa Mahakama Kuu ya Christchurch amesema Tarrant hajaonyesha kujuta na hiyo hata akibaki jela umri wake wote, adhabu hiyo haiwezi kutosha kufidia jinai zake. Aidha amesema katika hukumu hiyo ya maisha gerezani, Tarrant hatakuwa na haki ya kuomba kupunguziwa adhabu.

/3473317

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: