IQNA

Sheikh Mustafa Ismail akisoma aya za Qur'ani kuhusu Nabii Isa AS

14:14 - December 26, 2020
Habari ID: 3473494
TEHRAN (IQNA) – Taasisi ya Darul Qur'an ya Ujerumani imesambaza klipu ya qiraa ya Qur'ani kumhusu Nabii Isa Masih-Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake- ambaye Wakristo wengi wanaamini alizaliwa Disemba 25 katika siku ambayo ni maarufu kama Krismasi.

Katika klipu hiyo, qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Moustafa Ismail anasikika akisoma sehemu ya Aya ya 171 ya Sura Nisaa isemayo: "  ...Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha."

captcha