IQNA

21:36 - February 19, 2021
Habari ID: 3473665
TEHRAN (IQNA) – Kadhia ya Sudan kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel inapaswa kujadiliwa upya baada ya mabadiliko katika baraza la mawaziri, amesema mwanachama wa Baraza la Serikali ya Mpito.

Mohammad Al Faki Suleiman ameliambia Shirika la Habari la Anadolu kuwa: "Hapa tunazugumza kuhusu sera kamili ya kigeni ambayo inaambantana na maslahi yetu. Kwa msingi huo suala hili ( la kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel) linapaswa kujadiliwa upya."

Katika miezi mitatu ya mwisho wa mwaka uliomalizika wa 2020, nchi nne za Kiarabu za Imarati (UAE), Bahrain, Sudan na Morocco zilianzisha uhusiano rasmi na utawala haramu wa Kizayuni na Israel. Hatua hiyo ya kihaini na ya usaliti iliyofanywa na nchi hizo ambayo ni kushiriki kwenye mpango wa mapatano wa Kimarekani na Kizayuni, imeendelea kulaaniwa na kukosolewa vikali na Waislamu na wapenda haki kote duniani. Kitendo hicho cha nchi hizo za Kiarabu kinahesabiwa kuwa ni kuwasaliti Wapalestina ambao wanaendelea kupigania ukombozi wa ardhi zao zinazokoloniwa na Israel.

Kwa kuhadaiwa kuwa itapokea misaada ya kifedha ya Markeani,  serikali ya Sudan iliafiki kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kile kilichotajwa kuwa ni 'Mapatano ya Ibrahim'.

Pamoja na kuwa uamuzi kama huo haukutarajiwa kutoka kwa wakuu wa Sudan, si tu kuwa nchi hiyo haijapokea misaada ya  kifedha kama ilivyotarajia bali pia uamuzi huo umepelekea kushadidi hitilafu za kisiasa ndani ya Sudan.

Wananchi wa Sudan wamekasirishwa sana na utendaji kazi wa serikali ya mpito kwani walitaraji kuwa kwa kuondolewa utawala wa kidikteta wa al Bashir hali ingeboreka lakini sasa hali inazidi kuwa mbaya. Hivi sasa Wasudan waliowengi wamepoteza matumani kufuatia utendaji mbovu wa serikali ya mpito na kwa hivyo wamemiminika mitaani kubainisha malalamiko hayo. Wasudan wengi wanaamaini kuwa serikali ya mpito imeondoka katika mkondo wa malengo ya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani al Bashir.

3474021

Kishikizo: sudan ، israel ، uhusiano ، palestina
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: