IQNA

23:27 - February 01, 2021
Habari ID: 3473612
TEHRAN (IQNA)- Maulamaa na Maimamu wa Swala za Jamaa wasiopungua 200 nchini Mauritania wametoa Fatuwa inayorahamisha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawaa dhalimu wa Israel.

Kwa mujibu wa Fatuwa ya Maulamaa hao ni kuwa: Hatua yoyote ile inayolenga kuwa na uhusiano na utawala vamizi wa Israel unaoikalia kwa mabavu Palestina, Baytul-Muqaddas na maeneo yake ya kando kando, ni haramu na haijuzu.

Wakiwa katika kongamano lililofanyika katika mji mkuu wa Mauritania Nouakchott, maulamaa hao wamesisitiza kuwa, kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel maana yake  ni kuuunga mkono utawala huo ghasibu na kuwapatia himaya Wazayuni maghasibu na kuziunga mkono hatua zao kama mzingiro, mauaji na uangamizaji wao wa kizazi dhidi ya Wapalestina hatua  ambazo hazina uhusiano wowote na mchakato wa amani.

Fatuwa hiyo inatolewa katika hali ambayo, harakati za vyama mbalimbali vya siasa katika Bunge la Mauritania zenye lengo la kupasishwa sheria itakayopiga marufuku na kutambua kuwa ni uhalifu suala la kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel zinaendelea kushika kasi katika Bunge la nchi hiyo.

Katika miezi mitatu ya mwisho wa mwaka uliomalizika wa 2020, nchi nne za Kiarabu za Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco zilianzisha uhusiano rasmi na utawala haramu wa Kizayuni na Israel. Hatua hiyo ya kihaini na ya usaliti iliyofanywa na nchi hizo ambayo ni kushiriki kwenye mpango wa mapatano wa Kimarekani na Kizayuni, imeendelea kulaaniwa na kukosolewa vikali na Waislamu na wapenda haki kote duniani.

3951412

Kishikizo: mauritania ، palestina
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: