IQNA

Waziri Mkuu wa Uingereza aapa kupambana na Chuki Dhidi ya Waislamu

14:03 - November 20, 2025
Habari ID: 3481542
IQNA-Katika kikao cha maswali ya kila wiki bungeni, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer alitangaza kuwa chuki dhidi ya Waislamu ni jambo la kuchukiza na halina nafasi katika jamii.

Kauli yake ilitolewa kujibu swali la mbunge Afzal Khan wa chama cha Leba, aliyemuuliza hatua za serikali katika kukabiliana na kuongezeka kwa ubaguzi na Chuki Dhidi ya Waislamu nchini Uingereza.

Starmer alisema: “Chuki dhidi ya Waislamu ni ya kuchukiza… na haina nafasi katika jamii yetu. Kuongezeka kwa matukio haya lazima kushughulikiwe.”

Aidha, alisisitiza kuwa serikali yake inaongeza ufadhili wa kulinda misikiti na shule za Kiislamu kote nchini. Pia alieleza kuwa mfuko mpya utafuatilia chuki dhidi ya Waislamu, huku serikali ikiendelea kufanyia kazi ufafanuzi wa dhana ya chuki hiyo, sambamba na maadhimisho ya Mwezi wa Uelewa wa Chuki Dhidi ya Uislamu (IAM) mwezi Novemba.

3495467

Habari zinazohusiana
captcha