IQNA

Wanafunzi 185 wa Qur'ani Tukufu waenziwa Algeria

9:49 - February 23, 2021
Habari ID: 3473676
TEHRAN (IQNA)- Wanafunzi zaidi ya 185 wa Qur'ani Tukufu kutoka mikoa 26 ya Algeria ambao wamefanikiwa kuhifadhi Qur'ani katika mafunzo yaliyotolewa kwa njia ya intaneti wameenziwa katika sherehe iliyofanyika mjini Oran, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Sherehe hiyo imefanyika Februari 20 na kuhudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu serikalini maimamu wa misikiti, maulamaa na wanaharakati wa kijamii.

Amroush Mas'oud, Mkurugenzi wa Wakfu na Masuala ya Kidini Algeria amesema walioenziwa walishiriki katika kozi maalumu ya kuhifadhi Qur'ani kuanzia Julai 5 hadi Agosti 20, mwaka 2020.

Amesema kozi hiyo iliandaliwa na Chuo cha Al Shatibiya kwa mnasaba wa Siku ya Kitaifa ya Mashahidi wa Algeria.

Gavana wa jimbo la Oran Mas'oud Jari amesema wanafunzi walioenziwa katika hafla hiyo ni wanafunzi wa vyuo vikuu wanaosomea taaluma mbali mbali kama vile tiba, famacia, uhandisi, kemia na Tehama.

3955259

captcha