IQNA

21:44 - February 25, 2021
Habari ID: 3473682
TEHRAN (IQNA)- Taasisi za Kiislamu nchini Marekani zimelaani vikali hujuma dhidi ya msikiti unaojengwa mjini Strasbourg.

Kwa mujibu wa taarifa, watu wenye chuki dhidi ya Uislamu na kuandika maandishi yenye chuki yasemayo: “La kwa Uislamu, Rejeeni kijijini kwenu”.

Katika taarifa, Jumuiya ya Kiislamu ya Milli Gorus ambayo inaujenga msikiti huo imebainisha masikitiko yake kufuatia hujuma hiyo yenye chuki dhidi ya Uislamu.  Taarifa hiyo imesema hakuna hasara iliyopatikana katika jengo hilo lakini kitendo chenywe kina ujumbe mzito.  Msikiti huo unaojengwa unajulikana kama Eyyub Sultan, una ujenzi wake ukikamilika unatazamiwa kuwa msikiti mkubwa zaidi barani Ulaya.

“Tukio hilo linaashiria hali mbaya inayotawala Ufaransa hivi sasa. Kudunishwa matamshi yaliyo dhidi ya Waislamu aktika vyombo vya habari ni ishara kuwa maadui wameugana,” taarifa hiyo imesema.

Kijana mwenye umri wa miaka 21 amekamatwa na polisi baada ya kukili kutekeleza hujuma hiyo na anatazamiwa kufikishwa kizimbani baadaye.

Hayo yanajiri siku chache baada ya  Bunge la Ufaransa kuidhinisha sheria iliyo dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini humo.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, ambayo imepewa jina la “Sheria ya Kuimarisha Thamani za Kijamhuri” inalenga kukabiliana na mambo kadhaa yanayowahusu Waislamu kama vile mafunzo ya kidini, mitandao na kuoa wake wengi.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amependekeza sheria hiyo kwa ajili ya kukabiliana na kile alichokitaja ni 'Uislamu wa wanaotaka kujitenga.'

Msimamo huo wa Rais Macron umetajwa kuwa moja ya sababu ambazo zinachochea chuki dhidi ya Uislamu Ufaransa.

3474074/

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: