IQNA

Waislamu Marekani

Waislamu Houston Marekani wasusia futari kuonyesha mshikamano na Gaza

16:14 - March 17, 2024
Habari ID: 3478530
IQNA - Huko Houston, Marekani Waislamu wametangaza kususia hafla ya 25 ya kila mwaka ya Futari ambayo kulalmikia mwaliko kwa viongozi wa serikali.

Wanawataka waandalizi wa hafla hiyo kuondoa mwaliko huo kwa Meya John Whitmire, ambaye anatazamiwa kuwa mzungumzaji mkuu. Ususiaji huo unatokana na kutoridhishwa na meya na maafisa wengine wa jiji ambao wamekata kuchukua hatua kuhusiana na vita vya Gaza ambapo zaidi ya Wapalestina 32,000 wameuawa katika mashambulizi ya Israel tangu Oktoba 7.

Futari hiyo yam ji wa Houston inatarajiwa kufanyika Jumapili hii  na wito wa kususia ulirasimishwa kupitia barua ya wazi iliyotiwa saini na viongozi na mashirika zaidi ya 40 ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Kamati ya Kisiasa ya Umoja wa Waislamu na Baraza la Mahusiano ya Marekani na Uislamu la Houston Chapter, Axios iliripoti Ijumaa.

Barua hiyo inawakosoa waandaaji kwa kutoa mialiko kwa maafisa ambao hawajapaza sauti kuhusu kusitishwa kwa mapigano huko Gaza.

Licha ya upinzani uliopo, Meya Whitmire anatarajiwa kuhudhuria Futari hiyo. Msemaji wake ameelezea nia ya meya kuwa "uwepo wa umoja" katika chakula cha jioni.

Mashirika kadhaa, kama vile Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR) tawi la Houston, ambayo imekuwa ikihudhuria mara kwa mara na mara nyingi ikiongoza kamati ya maandalizi, imejiondoa ushiriki wao.

Al Noor Masjid, mwanachama mwanzilishi wa hafla hiyo, na Jumuiya ya Kiislamu ya Greater Houston, shirika kubwa la Kiislamu, pia wamejiondoa kwenye futari ya mwaka huu.

Vile vile, maswali kuhusu msimamo wa meya kuhusu kusitisha mapigano hayajashughulikiwa. Hapo awali Meya Whitmire alibainisha kuunga mkono utawala wa Israel na ana mpango wa kuongoza ujumbe nchini humo.

Ususiaji huo unakuja wakati baraza la jiji na meya wakitetea usitishwaji wa mapigano huku kukiwa na mashambulizi ya kijeshi ya utawala uliokaliwa huko Gaza, ambayo yanafanyika sanjari na Mwezi Mtukufu wa  Ramadhani.

Hali katika Gaza ni mbaya, huku maafisa wa Umoja wa Mataifa wakiripoti kuwa sehemu kubwa ya wakazi wako kwenye ukingo wa njaa.

Tamasha la Houston Iftar linatambuliwa kuwa mojawapo ya matukio makubwa zaidi ya aina yake katika taifa hilo, huku mahudhurio ya mwaka jana yalifikia takriban watu 2,300.

/3487602

captcha