Katika mahojiano na IQNA, Gholam Reza Amirkhani mtaalamu katika Maktaba ya Kitaifa na Makavazi ya Iran amesema safari hiyo ilikuwa ya kihistoria katika uhusiano wa Iran na Misri.
Amesema mwanazuoni wa ngazi za juu wa Kishia kutoka Iran Ayatullah Mohammad Taqi Qomi ambaye alikuwa amehamia Misri miaka kadhaa kabla ya safari hiyo, alijitahidi sana kustawisha uhusiano na ukuruba baina ya madhebu za Kiislamu.
Ayatullah Qomi alianzisha kituo kilichojulikana kama Dar al-Taqrib kwa lengo la kukurubisha madhehebu za Kiislamu ambapo aliwashirikisha wawakilishi wa madhehebu nne za Ahul Sunna. Amirkhani amesema harakati hizo za Ayatullah Qomi ziliungwa mkono na wanazuoni wa ngazi za juu wa Iran na Misri wakati huo akiwemo Ayatullah Borujerdi na Shekhe mkuu wa Al Azhar Sheikh Mahmoud Shaltut.
Ni kutokana na jitihada hizo ndio ujumbe wa Al Azhar ukafunga safari hadi Iran na kukutana na wanazuoni waandamizi wa Kishia nchini Iran katika miji ya Tehran, Mashhad, Qom na Isfahan.
Ujumbe huo uliandamana na qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Mahmoud Khalil al Husari ambaye alisoma Qur'ani katika baadhi ya mikitano.
Klipu hii hapa chini ni ya qiraa ya Sheikh al-Husari akiseoma aya katika Sura Ash-Shura katika moja vikao mjini Tehran.