IQNA

Waislamu Uingereza

Mbaguzi anaswa akimtusi Muislamu dereva wa basi jijini London

20:27 - August 09, 2024
Habari ID: 3479249
IQNA - Mwanamume mmoja amerekodiwa kwenye video akirusha maneno ya chuki dhidi ya Uislamu na kumtemea mate dereva wa basi Muislamu mjini London huku kukiwa na ongezeko la ghasia dhidi ya Waislamu katika nchi hiyo ya Ulaya.

Kundi la Documenting Oppression Against Muslims (DOAM) limesambaza video hiyo siku ya Alhamisi, na kuambatanisha maelezo yasemayo: "jambazi mbaguzi wa rangi ambaye amemtusi dereva Mwislamu jijini London."

Video hiyo inamuonyesha mwanamume huyo akimfokea mara kwa mara derive hiyo na kumtaja kuwa "gaidi Mwislamu". Pia alimtaka dereva ashuke nje ya basi na alionekana akitema mate na kugonga skrini ya basi hilo.

Tukio hili linakuja wakati wa machafuko nchini Uingereza, huku wazungu wenye misimamo mikali ya kibaguzi ya mrengo wa kulia wakiwalenga Waislamu, vikundi vya walio wachache na wahamiaji.

Ghasia hizo zilichochewa na madai ya uwongo yaliyoenezwa mtandaoni kwamba mshukiwa aliyekamatwa kwa mauaji ya watoto watatu Julai 29 huko Southport alikuwa Muislamu anayetafuta hifadhi.

Mamlaka imemtambua mshambuliaji huyo kuwa ni Axel Rudakubana, mwenye umri wa miaka 17 aliyezaliwa Cardiff na wazazi wa Rwanda na ambaye si Muislamu. Licha ya ufafanuzi huo, makundi ya watu wenye siasa kali za mrengo wa kulia wameendelea hujuma zao..

Kufikia Agosti 8, jumla ya watu 483 wamekamatwa, na mashtaka 149 yamefunguliwa kuhusiana na ghasia hizo katika miji na miji kote Uingereza.

Habari zinazohusiana
captcha